Habari za Punde

Wafanyakazi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Wapata Mafunzo ya Kujikinga na Maradhi ya Corona.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said, akizungumza wakati wa Mafunzo ya Elimu ya Maradhi ya Corona na Wafanyakazi wa Wizara hiyo yaliofanyika katika viwanja vya Wizara hiyo mazizini Wilaya ya Mjini Unguja.

Na.Mwanajuma Juma, Zanzibar
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali ikishirikiana na Chama cha Skaut Zanzibar wanaendelea kutoa mafunzo maalum ya dharura kuhusiana na mripuko wa maradhi ya Korona ili kuweza kuielimisha jamii kutoka na mripuko wa maradhi hayo.

Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo, katika ukumbi wa Wizara ya Elimu Mazizini Mjini Unguja, Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji na Utumishi wa Wizara hiyo Omar Ali Omar alisema, Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zimechukua hatua kubwa kuweza kutoa tahadhari  juu ya  ugonjwa wa korona usienee nchin.

Hivyo aliawataka wananchi nao kuchukuwa jitihada zao wenyewe kwa lengo la kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.

Aidha alifahamisha kuwa kitendo cha wanachama wa Skauti kufanya mafunzo kwa lengo la kuelimisha jamii ni cha kizalendo kwani wataweza kuokoa jamii kubwa kugokana na maambukizo ya maradhi hayo.

Alisistiza jamii kuzingatia maagizo ya Wataalamu wa Afya kwani janga la maradhi ya Korona sio la mtu mmoja pekee bali ni la dunia nzima.

Wakitoa Elimu ya maradhi korona na namna ya kujikinga, maafisa wa Elimu ya Afya Wizara ya Afya Zanzibar Mwanaisha Abdulrahman Mwarabu na Fatma Ali Khatib, wameeleza dalili kuu za ugonjwa huo ni kupata homa kali, kukohoa, chafya za mara kwa mara, kupata mafua makali, kuumwa na kichwa, vidonda vya koo na kupumua kwa shida

Hata hivyo wameeleza kuwa ungonjwa wa Corona unaweza kuepukika endapo jamii itafuata njia za kujikinga zilizoelezwa na  wataalamu ikiwa ni pamoja na  kunawa mikono kwa maji ya mtiririko na sabuni, kuepuka kukaa kwenye mikusanyiko ya watu, kuepuka tabia ya kupeana  mikono, kuepuka  kushika mdomo, pua na macho kabla ya kuosha mikono na kuepuka safari zisizo za lazima.
  
Nae Kamishna wa Skaut Mkoa wa Kaskazini Unguja  Ahmed S. Charinda amesema mafunzo hayo yatawajengea uelewa mkubwa juu ya janga lililo ikumba dunia na  kuahidi kuyafanyia kazi kwa kuwaelimisha jamii kama watakavyo elekezwa na wataalamu wa afya.
  
Akitoa shukurani, Afisa Mdhamin Wizara ya Elimu Pemba Mohamed Nassor Salim wamewashukuru Maafisa wa Afya kwa kuweza kutoa Elimu ambayo itawasaidia jamii kutokana na mripuko wa maradhi ya Korona.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.