Katibu Mkuu wa Wizara
ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki
Shemdoe ( wa pili kutoka kulia) akipatiwa maelezo na mtaalam wa TBS kuhusu upimaji wa bidhaa mbalimbali
unaofanyika katika maabara ya uhandisi mitambo,kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa
TBS Dkt Athuman Ngenya.
Mkurugenzi Mkuu wa
TBS Dkt Athuman Ngenya akisisitiza jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda
na Biashara Prof. Riziki Shemdoe wakati
wa ziara yake katika Shirika hilo hivi
karibuni.
Katibu Mkuu wa Wizara
ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki
Shemdoe (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TBS Dkt
Athuman Ngenya na watendaji wengine wa Shirika hilo mara baada ya ziara yake
katika Shirika hilo hivi karibuni.
Na
Roida Andusamile
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe amewataka watumishi wa Shirika
la Viwango Tanzania (TBS),kuepuka vishawishi katika utendaji kazi ili nchi iwe
salama na kuvutia wawekezaji zaidi.
Prof.
Shemdoe aliyasema hayo hivi karibuni alipotembelea TBS kwa mara ya kwanza baada ya kuteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli kuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.
Prof.
Shemdoe alisema ili kuwezesha biasharaTBS
inapaswa kufanya kazi kwa uadilifu na kuepuka urasimu ambao unakwamisha
biashara na kukatisha tamaa wawekezaji wapya.
“Tunapaswa
kushirikiana katika utendaji kazi na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kwa manufaa ya taifa,” alisisitiza Prof. Shemdoe
na kuongeza kuwa kwa sasa Tanzania iko nafasi ya 141 Duniani katika urahisi wa ufanyaji
wa biashara hivyo jitihada zaidi zinahitajika ili luwa katika nafasi nzuri
zaidi.
Alisema
Wizara ya Viwanda na Biashara ndiyo
inayotekeleza Blue Print kwa kuhakikisha
kuwa vikwazo vyote vya kibiashara vinaondolewa na kuweka mazingira mazuri ya
uwekezaji na biashara.
Awali
Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Athuman Ngenya akimkaribisha Katibu Mkuu
aliyeambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Ludovick Nduhiye, alimhakikishia
Katibu Mkuu kuwa Shirika hilo litaendelea kufanyakazi katika kiwango
kinachotakiwa licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa
vifaa vya kisasa vya maabara ili kwenda
sambamba na maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Dkt.
Ngenya alisema Shirika limeendelea kujizatiti katika kuhakikisha kuwa soko la
Tanzania linakuwa na bidhaa bora pekee ikiwa ni pamoja na kuendelea kufungua
ofisi mipakani na Kanda,ambazo zinatoa
huduma kwaa haraka tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo huduma za TBS
zilikuwa zinapatikana Dar es Salaam pekee.
Alisema mwezi Desemba 2019 Shirika lilifungua ofisi
mpya ya Kanda ya Magharibi mkoani Kagera ambayo kwa sasa inahudumia mikoa ya
Kigoma, Katavi na Rukwa. Kufunguliwa kwa kanda ya Magharibi kumefanya idadi ya
Kanda kwa sasa kufikia sita.
Alizitaja
kanda zingine zilizopo ni ya Kati Dodoma (Dodoma, Singida na Tabora), Nyanda za Juu
Kusini Mbeya (Mbeya, Iringa, Njombe, na
Songwe), Kanda ya Kusini Mtwara (Mtwara,Lindi na Ruvuma) Kanda ya Kaskazini
Arusha(Arusha,Kilimanjaro,Manyara na Tanga na Kanda ya Ziwa Mwanza (Mwanza,Kagera,Mara,
Geita, Simiyu na Shinyanga).
Dkt.
Ngenya pia alisema TBS imefungua ofisi katika viwanja vya ndege vya
Kilimanjaro, Dar es Salaam na Mwanza na katika Bandari za Mwanza, Tanga, Dar es
Salaam na Bagamoyo.
Alizitaja
ofisi za mipakani ni pamoja na Rusumo, Kabanga, Kasumulo,Tunduma,Holili,Horohoro,Namanga,
Sirari,Mutukula, Tarakea na Mtambaswala.
No comments:
Post a Comment