Habari za Punde

Wazazi na Walezi Kushirikiana Kuwalinda Watoto na Mambo Yanayowaathiri.

Na.Takdir Suweid -Maelezo Zanzibar.
Wilaya ya Magharibi B. 16-03-2020.
Wananchi wametakiwa kuunga mkono mikakati iliowekwa na Serikali ili kulinda na kuhifadhi haki za Watoto hapa nchini.
Wito huo umetolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Pangawe Mhe Khamis Juma Mwalim wakati alipokuwa akifunguwa Kongamano la kupinga vitendo vya Udhalilishaji kwa Wanafunzi wa Skuli ya Kijitoupele ‘A’.
Amesema Serikali imesaini Sheria ya Haki za Watoto ili kuweza kulinda na kuhifadhi haki zao.
Aidha amesema ili mikakati hiyo iweze kufanikiwa ni lazima  Wazazi na Walezi kushirikiana katika kuwalinda watoto na mambo yanayowaathiri ikiwemo vitendo vya udhalilishaji wanavyofanyiwa hasa wanapokwenda na kurudi Skuli na Chuoni.
Hata hivyo ameziomba Taasisi za Dini kushirikiana katika kuelimisha jamii ili kupiga vita vitendo vya udhalilishaji na Ukatili vinavyoendelea siku hadi siku.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Kijitoupele ‘A’ bi Mwanakombo Idrissa Makame amesema lengo la kuweka Kongamanao hilo ni kutoa elimu kwa Wanafunzi na Wanajamii juu ya Udhalilishaji ili kuweza kujuwa mbinu bora za kujikinga na vitendo hivyo.
Wakati huo huo Mh. Khamis amesema Uongozi wa Jimbo la Pangawe utaendelee kutoa elimu ya Ujasiriamali kwa Wanavikundi ili waweze kujiajiri na kuepukana na hali tegemezi.
Akifunguwa Mafunzo ya Siku 8 kwa Vikundi vya Wanawake vilivyomo katika Jimbo hilo huko Skuli ya Kijitoupe amesema kuna Wajasiriamali wengi hawana elimu jambo ambalo linawasababishia kupata hasara katika Biashara zao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.