Habari za Punde

Waziri Ummy awataka viongozi wa dini kupunguza mikusanyiko katika nyumba za ibada • Awataka wazazi kuwazuia Watoto wasizurure mitaani

Waziri waAfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na viongozi wa dini kuhusu majukumu yao katika kuzuia maambukizi ya Corona nchini, kwenye mkutano ulofanyika Jijini  Dar es salaam.
Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu, Abubakari Zuberi akiwa kwenye mkutano wa viongozi wa dini.

Baadhi ya viongozi wa dini wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.Mhe. Ummy Mwalimu wakati akizungumza na viongozi wa dini jijini Dar es Salaam.



Serikali imewataka viongozi wa dini kuchukua tahadhari zaidi katika Sikukuu ya Pasaka kwa kufanya ibada fupi na kupunguza mikusanyiko katika nyumba za ibada sambamba na kuwaelimisha waumini jinsi ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.



Kauli hii ameitoa leo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati alipokutana na viongozi wa dini ambapo mada kuu ni ' Majukumu ya viongozi wa dini katika Kuzuia maambukizi ya Corona.’

Katika mkutano huo, Waziri Ummy Mwalimu amewataka viongozi wa dini kufanya ibada katika mazingira salama Kama vile kukaa mbali zaidi ya mita moja, kufanya ibada katika mazingira ya kutoshikana mikono, kupunguza ukaribu wakati wa kuingia msikitini au kanisani.

Pia, Waziri amewataka viongozi wa dini kuwasisitiza waumini kwamba wanapaswa kunawa mikono kwa maji Safi natiririka, kutumia vitakasa mikono na amewataka waendelee kumuomba mwenyezi Mungu kuwaepusha Watanzania na ugonjwa huo.

“Ninyi viongozi wa dini mnaaminika kwa kutoa taarifa sahihi na hivyo kupunguza taarifa ambazo si za kweli katika jamii.

Akizungumzia mwenendo wa Hali ya maambukizi nchini, Waziri Ummy amesema kuwa maambukizi ya virusi vya Covid-19 yaliletwa na wasafiri kutoka nje ya nchi, Sasa yameingia katika hatua ya pili na kwamba wananchi wameanza kuambukizana wenyewe kwa wenyewe ndani ya nchi.

“Unakuta mtu ameambukizwa virusi vya corona lakini ukimuuliza amepataje, hajui hivyo jambo la msingi nasisitiza viongozi wetu muepuke mikusanyiko ili tuweze kujikinga na ugonjwa huu,” amesema Ummy Mwalimu.

Katika hatua nyingine, amewataka wazazi kuwazuia Watoto kutotembea ovyo kipindi hiki ambacho wapo likizo kutokana na juhudi za Serikali za kukabiliana na ugonjwa wa Corona.

“Leo ni Alhamisi Kuu, kesho ni Ijumaa Kuu Kuna watu wanatoka mijini na kwenda vijijini, viongozi wetu wa dini wa dini naomba mtusaidie, watu wanapaswa kujitafakari Kama Kuna ulazima wa kwenda vijijini, kwa sababu wanaokwenda huko kuwaambukiza Corona wazee na walezi wetu. Sisi tunashauri kwamba kipindi hiki msiende vijijini,” amesema Waziri Ummy.

Vile vile, amewataka wazazi na walezi kuwalinda Watoto wasizurure kipindi hiki na kwamba si wakati wa watoto kwenda kwa mjomba Wala shangazi kwani Serikali ilifunga shule ili wakae nyumbani katika mazingira salama.

Naye Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu Abubakari Zuberi amesema watawahimiza waumini kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya jinsi ya kujikinga ugonjw awa Corona pamoja na wazazi kuwalinda watoto wasizurure mitaani Kama alivyoagiza Waziri UmmyMwalimu.

Pia, Sheikh Mkuu, Zuberia amewataka viongozi wenzake wa dini kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya Kama vile kunawa mikono, kukaa mbali zaidi ya mita moja na kuzuia mikusanyiko ili Kukabiliana na ugonjwa wa Corona nchini.

“Naomba mwezi huu wa Ramadhani, viongozi wenzangu mzingatie maelekezo ya wataalamu, kukaa mbali na zaidi ya mita moja na kufanya ibada katika mazingira salama,” amesema Sheikh Mkuu, Zuberi.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Askofu  Dkt. Alinikisa Cheyo amesema maelekezo ya waziri pamoja na wataalamu watayazingatia ili kukabiliana Covid-19.
“ Sisi viongozi wa dini tunakwenda kutekeleza maelekezo ya wataalamu, pia Tutaendelea kufanya maombi ili mwenyeziMungu awalinde watu wetu. 

Pia kuhusu wazazi wanatakiwa kuwalinda Watoto, Hilo tumelibeba na tunakwenda nalo,” amesema Askofu Dkt. Cheyo


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.