Habari za Punde

Baadhi ya hatua zilizotangazwa na rais Uhuru Kenyatta za kukabiliana na janga la corona.

Rais Uhuru Kenyatta alisema Wizara ya Afya na huduma za umma itaanzisha hazina ya kuwasaidia wafanyakazi wa Afya wanaokabiliana na mlipuko wa virusi vya corona


1.Wizara ya Afya na huduma za umma itaanzisha hazina ya kuwasaidia wafanyakazi wa         Afya wanaokabiliana na mlipuko wa virusi vya corona                                                          
2. Wizara ya elimu itachukua hatua kuwalinda wanafunzi kutokana na athari mbaya za hatua zilizochukuliwa kukabiliana na Covid-19
3. Mamlaka ya usambazaji wa tiba nchini Kenya itaondoa masharti ya ununuzi wa vifaa vya kujilinda dhidi ya Covid-19 kwa takriban miezi mitatu ili kurahisishia kaunti kununua vifaa hivyo.
4. Nyumba za watu wasiojiweza jijini Nairobi zitafaidi kutokana na fedha zilizotengwa na serikali kusaidia familia zisizojiweza
5.Bunge litapitisha tena mapendekezo na miswada kuhusu vichocheo vya uchumi.
6. Ili kuhakikisha msaada unagawanywa kwa njia salama, mfuko wa hali ya dharura wa kukabiliana na Covid-19, Kenya na mashirika mengine ya usalama yatashirikiana kuratibu miradi kama ule wa Adopt a Needy Family, ambapo raia wa Kenya wanasaidiana kipindi hiki cha janga kuhakikisha hatua zinachukuliwa bila kufuata urasimu
7.Afisa yeyote wa polisi atakayekiuka sheria wakati anatekeleza hatua za kukabiliana na usambaaji wa virusi atakabiliwa na mkono wa sheria.
Awali Bwana Kenyatta alisema , kwa mujibu wa agizo la kuepuka maeneo yenye mikusanyiko mikubwa, watu waepuke maeneo yenye umati wa watu, agizo lake likisema watu :
  • waepuke mikusanyiko ikiwemo maeneo ya kuabudu
  • wapunguze mikusanyiko ya kijamii mkiwemo harusi na mazishi, na masharti hayo yazingatiwe mara moja na wanafamilia
  • waepuke maeneo yenye msongamano wa watu mkiwemo maduka ya jumla na maeneo ya burudani
  • wapunguze mikusanyiko katika maeneo ya usafiri wa umma na kwingineko iwezekanavyo.
  • Kuwepo ukomo wa wageni wanaotembelea wagonjwa waliolazwa katika hospitali za umma na za kibinafsi.
  • Chanzo cha Habari BBC NEWS.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.