Habari za Punde

Naibu Waziri wa Elimu Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said Ashiriki Mkutano wa Kimataifa kwa Njia ya Mtandao Kujadili Namna ya Kushirikiana Katika Sekts ya Elimu.

 Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Mhe Simai Mohammed Said , akiwa na Naibu Katibu Mkuu Utawala na Uendeshaji wa Wizara hiyo, mw Abdullah Mzee Abdullah wakishiriki mkutano wa Kimataifa wa saa moja  na nusu kupitia mtandao "VIRTUAL DISCUSSION" hapo ofisini kwake Mazizini Mjini Unguja.

Mhe Simai ameshiriki mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, ambao una lengo la kujadiliana namna ya kushirikiana kwa sasa juu ya janga la covid-19 katika suala la Elimu.

Aidha mkutano huo,  umewashirikisha Mawaziri wa Elimu wa Bara la Afrika, Mawaziri wa Pakistan, Mnyanmar, Cambodia na Maldives.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.