Habari za Punde

PROF.GABRIEL AWATAKA WAFANYAKAZI SEKTA YA MIFUGO KUTEKELEZA WELEDI KWA KUWATETEA WAFUGAJI

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza hilo akizungumza katika kikao kazi cha Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika Jijini Dodoma.
Katibu wa Baraza hilo Bw.Andrew Ponda akisoma maazimio kwenye kikao kazi cha Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wizara hiyo Bw.Stuart Mgunya,akizungumza kwenye kikao kazi cha Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza hilo akieleza jambo katika kikao kazi cha Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika Jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utawala, Rasilimali Watu Sekta ya Mifugo Bi. Teddy Njau akizungumza katika kikao kazi cha Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika Jijini Dodoma.

Mchumi kutoka wizara ya mifugo Bw.Francis Makusaro akitoa taarifa kwenye kikao kazi cha Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza hilo akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kikao kazi cha Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika Jijini Dodoma.

Na.Mwandishi wetu, Dodoma                           
Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya Mifugo limeazimia kuwatetea wafugaji ili kutovunja sheria,kanuni na kuwa fanya kutambua haki zao katika kutimiza malengo katika shughuli zao. 

Azimio hilo limetolewa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza hilo katika kikao kazi cha Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika Jijini Dodoma.

Prof. Gabriel amesema kuwa sekta hiyo imejipanga vema kuchangia katika uchumi wa viwanda kwa kuzalisha malighafi ya kutosha itakayotumika katika viwanda vya hapa nchini katika kusukuma uchumi wa kati. 

"Watumishi wote wa sekta hii mnatakiwa kufanya kazi bila uzembe na kutoleta ubadhilifu katika sekta hii ili kulinda weledi wenu" amesema
 Prof. Gabriel. 

Aidha katika kikao hicho Prof.Gabriel ameeleza kuwa wameazimia kutekeleza majukumu ya wizara katika kiwango bora kinacho hitajika ili kuleta ubora katika kuwahudumia wananchi. 

Prof. Gbriel ameweka wazi kuwa kila mfanyakazi katika sekta hiyo atakatwa kiasi cha shillingi 10,000/= ili kuweza kuchangia katika mfuko wa faraja unaosaidia katika matatizo mbalimbali yanayomkuta mfanyakazi. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wizara hiyo Stuart Mgunya amesema kuwa wafanyakazi wanahaja ya kuwa pamoja katika kuboresha ustawi wa watumishi ili kufikia malengo yao katika kutimiza majukum yao. 

Mgunya ametoa wito kuwa kupatikane siku moja ya kuweza kuwashika mkono wastaafu katika wizara hiyo ikiwa ni ishara ya shukrani na pongezi kwa utumishi wao ulio tukuka katika kutumikia taifa. 

Naye Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utawala, Rasilimali Watu Sekta ya Mifugo  Teddy Njau amesema sasa ni wakati muhimu watumishi kujiunga katika mfuko wa faraja wenye lengo wa kusaidiana katika wizara hiyo.

Katika kikao hicho baraza hilo limemchagua Andrew Ponda kuwa Katibu wa Baraza na Katibu Msaidizi ni Suzanna Silayo ambao watakuwa madarakani kwa miaka mitatu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.