Habari za Punde

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 15.05.2020: Silva, Matondo, Lewandowski, Coutinho, Mertens, Adams, Foyth

Mkataba wa David Silva mwenye umri wa miaka 34, kwa Manchester City unakamilika Juni 30 lakini Mhispania huyo anayecheza safu ya kati,yuko tayari kuongeza mkataba huo hadi mwisho wa msimu, kabla ya kufunganya virago. (Times - subscription required)
Manchester United wamekuwa wakimsaka Schalke na Rabbi Matondo na huenda wakamnunua mchezaji huyo wa miaka 19, wakishindwa kumsainisha mshambuliaji wa Borussia Dortmund na England, Jadon Sancho, 20. (Manchester Evening News)
Mchezaji Dries Mertens anayenyatiwa na Chelsea anampango wa kuhamia ligi ya Italia ya Serie A mkataba wake na Napoli utakapokamiliaka, Inter Milan pia inamtaka kiungo huyo mshambulizi wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 33. (Mail)
Mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowsk
Mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski, 31, has amaemshauri mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland,19 - ambaye anang'ang'aniwa na Manchester United na Real Madrid - kuendelea na ukuzaji wa talanta yake Borussia Dortmund. (Metro)
Wakala wa kiungo wa kati wa Brazil Philippe Coutinho,27, amesema hajafanya mazungumzo na klabu yoyote kumhusu mchezaji huyo wa Barcelona, ambaye yupo kwa mkopo Bayern Munich. (Talksport)
Mshambuliaji wa Southampton Muingereza Che Adams anakaribia kuuzwa kwa £10m Ama chini ya hapo- licha ya Leeds United kukubali ada ya £19m kumnunua kiungo huyo wa miaka 23, mwezi Januari kabla ya kubadilia nia yao. (Football Insider)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.