Habari za Punde

Ahukumiwa Miaka Tisa Kwa Kosa la Udhalilishaji


Na Halima Mohammed
KIJNA wa miaka 19 . Nassor Mohammed Makame, mkaazi wa Kilimahewa wilaya ya Mjini Unguja, amehukumiwa kutumikia Chuo cha Mafunzo kwa muda wa miaka tisa, kwa kosa la kumwingilia kinyume cha maumbile msichana wa miaka 16.



Hukumu ya mshitakiwa huyo ilitolewa na hakimu wa mahakama ya Mkoa Vuga chini ya Hakimu Makame Khamis Ali baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashataka.

Mshitakiwa huyo awali alipandishwa kizimbani hapo kujibu tuhuma tatu zikiwemo ya Kutorosha, Kubaka na kulawiti ambapo tuhuma mbili zilishindwa kuthibitisha kosa na kosa la ulawiti ndio aliloshitakiwa nalo na kumpatia adhabu hiyo.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Makame alisema, kutokana na ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashitaka, umeweza kuthibitisha kosa la kulawiti na makosa ya kubaka na kutorosha yameshindwa kuthibitishwa, na hivyo alifahamisha kwamba, kwa makosa hayo mahakama imemwachilia kwa faida ya shaka

Mapema Mwendesha Mashitaka Omar Makungu, Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa, ili iwe fundisho kwake na kwa wengine.

Mshitakiwa huyo alidaiwa kutenda kosa hilo Machi 8 mwaka jana kati ya majira ya saa 1:00 hadi saa 3:00 za usiku huko Ziwatuwe wilaya ya Mjini mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.