Habari za Punde

Kuna idadi kubwa ya matukio ya udhalilishaji Zanzibar

 Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Zanzibar Univeristy Dkt,Sikujua Omar Hamdan akiwasilisha ripoti ya matukio ya udhalilishaji kwa watoto Zanzibar kuelea kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Africa ambao uwasilishwaji huo umefanyika katika ukumbi wa watu wenye ulemavu kikwajuni Weles Unguja.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia kwa umakini uwasilishwaji wa taarifa hio.

Muhammed Khamis-TAMWA-ZNZ

Wakati tukielekea katika siku ya maadhimisho ya Mtoto Africa ifikapo Julai 16 mwaka huu Asasi za kirai visiwani Zanzibar zimesema kuna idadi kubwa ya matukio ya udhalilishaji kwa watoto visiwani Zanzibar kutoka mwaka 2017 mpaka sasa.

Akiwasilisha ripoti ya asasi hizo Mhadhiri kutoka Chuo kikuu cha Zanzibar University (ZU) alisema kuna matukio yapatayo (1,490) katika maeneo mbali mgali ya Unguja na Pemba.

Akitolea ufafanuzi wa kesi hizo, alisema  kesi ambazo zimetolewa hukumu kutoka mwaka  2017 hadi sasa ni  (404)  wakati kesi (704 ) zinaendelea na upepelezi na kesi (266) watuhumiwa hawakukutwa na hatia na kesi (59) zilikutwa na hatia.

Akitaja sababu za uwepo wa matukio hayo aliema ni pamoja na baadhi ya wanajamii kutokua makini na malezi ya watoto wao sambamba na kuwanunua vitu visivyokua muhimu na vinavyoweza kujenga ushawishi kwa watoto.
Pia alisema baadhi ya wanajamii kutokua na uelewa ipasavyo kuhusu matendo ya udhalilishaji na kuhisi kuwa ni vitu vya kawaida na ndio maana hushindwa kuwadhiti na kuwafuatilia watoto wao majumbani.

Alieleza kuwa imekua kawaida kwa baadhi ya wazazi au walezi kuwafungulia milango watoto wao wa kike saa tano za usiku kwa kisingizio cha kujisomea elimu ya dhiada kwa marafiki zao.

Akifafanua zaidi alisema mazingira hayo nayo pia ni sehemu hatarishi kwa watoto kufanyiwa udhalilishaji na kwamba wazazi au walezi wanapaswa kukataa mwenendo wa watoto wao.

Awali Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria wanawake Zanzibar (ZAFELA) Jamila Mohamed alisema ipo haja kubwa wakati Africa ikielekea kuadhimisha siku hio jamii kubadili tabia na kutambua umuhimu wa mtoto.

Alisema kuwekwa kwa siku hio mahsusi ililenga kutambua umuhimu wa mtoto wa Africa na kwamba wanapaswa kutunzwa na kuenziwa muda wote.

Alisema mtoto kama mtu mwengine anapaswa kupatiwa haki zake zote za msingi kama wanavopatiwa wengine wote.
Meneja miradi kutoka Chama cha Waaandishi wa habari wanawake TAMWA-ZNZ Asha Abdi alisema kuna mazingira ambayo watetezi wa haki za watoto wamekua wakikutana nayo hususani kwenye kufuatilia kesi zao.

Alisema imekua kawaida kwa baadhi ya maafisa wa polisi kuwataka wanaofika kituoni kuwafuatilia na kuwapeleka polisi wale watu ambao wanahisi wamewatendea mabaya watoto wao.

Aidha alisema hata katika uandishi wa ripoti maalumu ya matukio hayo inayotolewa kwenye vituo vya polisi (PF3) haiweki wazi ni kitu gani mtoto anataka kupimwa anapokwend akituo cha afya.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.