Habari za Punde

Mwanachama wa Kwanza Mwanamke Ajitokeza Kugombea Urais wa Zanzibar Akiwa wa 11 Kuchukua Fomu Hizo leo.


Kada wa Chama cha Mapinduzi Mhe. Mwatum Mussa Sultan akiwa Mwanamke wa Kwanza kuchukua Fomu ya Kugombea Urais wa Zanzibar akiwa ni Mwanachama wa 11 kujitokeza kuchukua Fomu leo katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar. Akionesha mkoba ukiwa na Fomu za Kugombea Urais wa Zanzibar baada ya kukabidhiwa akiwaonesha Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo leo. 
Katibu wa Idara ya Oganizesheni ya CCM Zanzibar Ndg. Galos Nyimbo akimkabidhi Fomu za kugombea Urais wa Zanzibar Kada wa CCM Mhe. Mwatum Mussa Sultal, alipofika Afisi za CCM Kisiwandui kuchukua fomu akiwa ni mwanamke wa kwanza kujitokeza katika kinyanganyiro hicho cha kuwania Urais wa Zanzibar.
Katibu wa Idara ya Oganizesheni ya CCM Zanzibar Ndg. Galos Nyimbo akimkabidhi Fomu za kugombea Urais wa Zanzibar Kada wa CCM Mhe. Mwatum Mussa Sultal, alipofika Afisi za CCM Kisiwandui kuchukua fomu akiwa ni mwanamke wa kwanza kujitokeza katika kinyanganyiro hicho cha kuwania Urais wa Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe. Mwatum Mussa Sultan akitoka katika jengo la Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar baada ya kukamilisha zoezi la uchukuaji wa fomu ya Urais akielekea katika eneo lililoandaliwa kwa ajili ya kuzungumza na Waandishi wa habari Zanzibar.


MWANTUMU Mussa Sultani amekuwa mwanamke wa kwanza kujitokeza katika ofisi Kuu za chama zilizopo Kisiwandui mjini Unguja kuchukuafomu za kuomba kupewa ridhaa na Chama Cha Mapinduzi(CCM)kugombea nafasi ya  urais wa Zanzibar.

Kada huyo wa CCM aliingia katika ofisi hizo za chama majira ya saa ya tano za asubuhi baada ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji Professa Makame Mbarawa kuchukua fomu hiyo.

Baada ya kuchukua fomu hiyo Mwantumu alisema kwa upande wake amekuwa mwanamke wa kwanza kujitokeza kutia nia ya kuomba kupewa ridhaa na CCM kugombea nafasi hiyo.

Alisema akiwa kama mwanamke amekuwa wa kwanza kuwahamasisha wanawake wenzake kujitokeza
kutia nia ya kugombea nafasi hiyo kupitia CCM.

Kada huyo alikipongeza Chama kwa ukomavu wake wa demokrasia ya kuwaruhusu makada wake wa jinsia zote kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kupitia chama.

Mwantumu aliongeza kwa kukipongeza CCM kwa kuweka wazi na kuwepo kwa demokrasia kwa wanachama wa kuchukua fomu ya kugombea kwa nafasi yeyote ile bila ya kubagua jinsia.

"Sababu mimi ni jinsia ya kike lakini nimejitokeza kugombea nafasi hii ya urais kwa hivyo ninawaambia wanawake wenzangu wasiogope wachukue fomu na kwamba hichi chama ni chetu sote hivyo tuwajibike kuchukua fomu,"alisema Mwantumu

Alisema wanawake wajitokeze kuchukua fomu kwa wingi ikiwemo nafasi ya urais,Ubunge,Uwakilishi na udiwani tujitokeze kwa sababu tunataka usawa wa nafasi ya 50 kwa 50,"alisema

Katika maelezo yake alisema endapo wanawake hawatajitokeza kuchukua fomu hawataipata asilimia ya usawa wa 50 kwa 50.

"Namuomba Mwenyezi Mungu anisaidie katika safari yangu anipe moyo wa busara,hekima,imani ili niweze kukamilisha majukumu yangu,"alisema

Aliwataka wanawake nchini kuendelea kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ilikufikia asilimia 50 kwa 50 katika vyombo vya kufanya maamuzi.

Mwanamke huyo alisema amechukua fomu hiyo ili kuwahamasisha wanawake wengine wajitokeze katika kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kama walivyo wanaume.

"Nachukua nafasi hii kumuomba Mwenyezi Mungu anisimamie katika safari yangu hii ya kuomba ridhaa
ya kuwa Rais wa Zanzibar", alisema Mwatum.

Pamoja na hayo aliwaomba radhi waandishi wa habari kuwa hatoweza kutoa maelezo mengi mpaka pale atakapokamilisha kujaza fomu hiyo.

Kabla ya kujitokeza mwanamke huyo kuchukua fomu katika ofisi hizo kada mwingine alijichomoza ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji Professa Makame Mbarawa.

Baada ya kuchukua fomu Waziri Profesa Mbarawa alisema anamuomba Mwenyezi Mungu amsimamie na amfanyie wepesi katika safari hiyo aliyoanza.

"Ninachukua nafasi hii kuzungumza na watanzania kuwa tumeianza hii shughuli dua zao ni muhimu tuombe kwa Mungu atusimamie na twende vizuri," alisema

Alisema jambo la mwisho anawaomba watanzania kuendelea kumuomba Mungu ili aweze kufungulia milango kwa jambo wanalolitaka.

Kada mwingine alijitokeza kuchukua fomu hiyo ni Haji Rashid Pandu ambapo baada ya kuchukua fomu alisema endapo atapata ridhaa ya kugombea atafanya mabadiliko kwa Zanzibar hasa katika kilimo.

Alisema anataka kufanya mapinduzi ya kilimo kwa kufanya uzalishaji uwe mkubwa na kwamba uzalishaji huo utaongezeka kutoka na na kuwa jembe la mkono limepitwa na wakati hivyo itahitajika mabadiliko na hatua hiyo itasaidia sana kuzalisha kwa wingi na kuinufaisha nchi.

"Tutanufaika kupata chakula cha kutosha kwa kuuza mazao nje ya nchi tutanufaika kwa viwanda vyetu kwa kupata mzunguko mzuri wa malighafi na kufanya uzalishaji mkubwa bila ya kusimama kwa mwaka mzima na kwamba hiyo ndio nia yangu," alisema

Alisema nia yake ya pili ni kufanya mapinduzi ya kiuchumi katika vijiji ambavyo vimedhorota sana katika uzalishaji wa mali na kuwa anakusudia kuwa nyenzo zipo malighafi zipo na fursa zipo lakini bado havijafanya kazi ipasavyo.

"Nasema havijafanya kazi ipasavyo kutokana na kuwa havijashughulikiwa kama nitapewa ridhaa uwezekano huo ni mkubwa nitafanya hivyo kwa maslahi ya taifa makubwa,"alisema

Kada mwingine aliyechukua fomu hiyo Dk.Abdulhalim Mohamed Ali alisema ameona kuwa umefika muda wa kuingia katika kinyanganyiro hicho cha kuomba ridhaa kwa CCM kugombea nafasi hiyo ili kusaidia kusukuma gurudumu la maendeleo lifike mbele zaidi.

Alisema kutokana na uwezo aliokuwa nao kwa umri wake na uzoefu wake aliyonao kwa Zanzibar ataweza kuwasaidia wananchi kuwapa matumahini mazuri kwa kuwapatia maendeleo.

"Ninahidi kushirikiana na wenzangu na kufanya kazi kwa pamoja nadhani kwa maneno hayo yanatosha kutokana na kuwa fomu hii sijaisoma lakini baada ya kuzisoma fomu hizi nitazungumza,"alisema

Akijibu swali la waandishi habari kuhusu muono wake wa maendeleo ya Zanzibar alisema yeye msimamo wake akipata ridhaa ya CCM atahakikisha anasukuma kwa haraka maendeleo ya Zanzibar kutokana na kuwa maendeleo yapo lakini yanakuja kwa taratibu.

"Nina amini kuwa maendeleo yatafikiwa kama navyotaka yawe na kwamba wananchi naomba mniamini kama wananchi watanipatia kura na hakika tutaleta maendeleo ya haraka kwa kujiamini,"alisema   

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.