Habari za Punde

MASOLI NAE KUTIA NIA UDIWANI KATA YA SONGE

Na Hamida Kamchalla, KILINDI.Mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe mkoani Tanga Dege Masoli ametia nia ya kuwania kiti cha Udiwani kwa tiketi ya CCM katika kata ya Songs, Wilaya ya Kilindi, mkoani humo.Akiongea na mwandishi wa habari hii kwa njia ya simu akiwa katika kata yake jana Masoli alisema kuwa alichukua fomu ya kuwania nafasi hiyo juzi julai 16 na kuirejesha jana julai 17 na kueleza kwamba ameamua kutia nia na ikibidi kupata ridhaa ya chama na baadae kusimama akiwa Mgombea wa kiti hicho kupitia chama hicho ili kuipigania kata hiyo ambayo ina changamoto kadhaa.Masoli alisema kuwa kata hiyo ni moja ya kata ambazo zina changamoto nyingi zilizoyokana na utekelezaji mdogo wa uongozi uliopita hivyo ameamua kukiwania kiti cha udiwani ili kutatua changamoto hizo na kuiweka kata hiyo na wananchi wake katika maisha bora kwa kutekeleza ilani."Nimechukua fomu jana tarehe 16 na leo hii narudisha, nimeamua kuwania kiti hiki kutokana na changamoto nyingi zilizopo hapa, utakalazaji wa ilani ulishindwa kufanyika katika kipindi kilichopita hivyo nikaona vema niipiganie kata yangu kwa kugombea nafasi hii" alisema.Masoli aliongeza kuwa "Endapo nitaipata nafasi hii ndani ya chama na nikisimamishwa mgombea kwenye uchaguzi mkuu, nawaomba wananchi wanikopeshe kura zao za ndiyo na mimi nitawalipa maendeleo ndani ya kata yao" alisisitiza.Naye Katibu wa kata hiyo Hassani Mtambi alisema kuwa mpaka kufikia jana majira ya saa tano asubuhi walishapokea na kuwapatia fomu watia nia wa kugombea udiwani nane na kuongeza kuwa wanatarajia kutoa fomu hizo kwa watia nia 11mpaka kufikia saa kumi jioni kulingana na idadi ya maombi hayo.Mtambi aliwataja watia nia waliokwisha chukua fomu kuwa ni Twaha Mbwego, Swalehe Mganga, Abdallah Kisarazo, Dege Masoli, Mohamedi Makengwa, Mohedi Mazige, Samwel Loramatu na Alhaji Mohamedi Zambo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.