Habari za Punde

Mkutano wa Mapokezi na Kumtambulisha Mgombea Urais wa Zanzibar Kwa Tiketi ya CCM Uliofanyika Kisiwani Pemba 19-7-2020.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasalimia Wananchi wakati akiwasili katika viwanja vya Tibirinzi Chakechake Pemba, katika hafla ya mapokezi na kumtambulisha Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dkt. Hussein Mwinyi. (hayupo pichani) 
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed, akiwa na Viongozi meza kuu na (kulia kwa Rais) Mgombea Urais wa Zanzibar CCM Mhe.Dkt. Hussein Mwinyi na (kushoto kwa Rais) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi wakiwa wamesimama wakati ukiimbwa Wimbo wa Ukombozi katika mkutano wa Mapokezi na Kutambulishwa Mgombea wa Urais Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi, uliofanyika katika uwanja wa Tibirinzi Chakechake Pemba.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed, akiwa na Viongozi meza kuu na (kulia kwa Rais) Mgombea Urais wa Zanzibar CCM Mhe.Dkt. Hussein Mwinyi,Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Mama Asha Suleiman Iddi, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Bi.Leila Ngozi na Mke wa Mgombea Urais wa Zanzibar Mama Maryam Mwinyi  na (kushoto kwa Rais) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Balozi Seif Ali Iddi na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe.Zuberi Ali Maulid,  wakiwa wamesimama wakati ukiimbwa Wimbo wa Ukombozi katika mkutano wa Mapokezi na Kutambulishwa Mgombea wa Urais Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi, uliofanyika katika uwanja wa Tibirinzi Chakechake Pemba.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akikabidhiwa risala ya Wananchi wa Mikoa Miwili ya Pemba wakati wa hafla ya Mapokezi na Mkutano wa Kumtambulisha Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dkt.Hussein Mwinyi (hayupo pichani) mkutano huo umefanyika katika uwanja wa Tibirinzi Chakechake Pemba.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisoma risala ya Mikoa miwili ya Pemba wakati wa hafla ya mapokezi na kutambulishwa kwa Mgombea Urais wa Zanzibar, mkutano uliofanyika katika viwanja vya Tibirinzi Chakechake Pemba.na kushoto Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.Mhe.Zuberi Ali Maulid.
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ole Pemba  CUF kwa sasa amejiunga na Chama Cha Mapinduzi Mhe. Juma Hamad Omar, akizungumza wakati wa hafla ya mkutano wa mapokezi na kutambulishwa kwa Mgombea Urais wa Zanzibar  Mhe.Dkt. Hussein Mwinyi.(hayupo pichani) mkutano huo umefanyika katika viwanja vya Tibirinzi Chakechake Pemba.

Mgombea Urais wa  Zanzibar  Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akisalimiana na Mhe. Juma Hamad Omar aliyekuwa Mbunge wa Ole CUF, kwa sasa amejiunga na Chama cha Mapinduzi,   
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Wawi Pemba kwa sasa amejiunga na CCM Mhe. Mohammed Juma Nwali, akizungumza wakati wa mkutano wa kutambulishwa kwa Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dkt. Hussein Mwinyi.(haytupo pichani) mkutano huo umefanyika katika viwanja vya Tibirinzi Chakechake Pemba.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsalimia na kumpongeza aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Wawi Pemba CUF kwa sasa amejiunga na CCM Mhe. Mohammed Juma Nwali, baada ya kumaliza kuzungumza wakati wa hafla ya mkutano wa mapokezi na kutambulishwa Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dkt. Hussein Mwinyi. 
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chakechake Pemba CUF kwa sasa amejiunga na Chama cha Mapinduzi Mhe. Yussuf Kaiza, akizungumza wakati wa hafla ya mkutano wa kutambulishwa na mapokezi ya Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dkt. Hussein Mwinyi , mkutano huo umefanyika katika uwanja wa Tibirinzi Chakechake Pemba.
Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi akizungumza wakati wa mkutano wa cmapokezi na kumtambulishwa Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dkt. Hussein Mwinyi kwa wananchi wa Pemba katika viwanja vya Tibirinzi Chakechake Pemba.

WALIOKUWA Wabunge wa Chama cha CUF na sasa Wamejiunga na CCM, wakifuatilia hutuba ya mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dkt. Hussein Mwinyi(hayupo pichani) wa kwanza kulia aliyekuwa Mbunge wa Chakechake Mhe. Yussuf Kaiza, Mhe. Juma Hamad Omar aliyekuwa Mbunge wa Ole na Mohammed Juma Nwali aliyekuwa Mbunge wa Wawi Pemba, wakifuatilia mkutano huo.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.