Habari za Punde

Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Pombe Magufuli Aongoza Mkutano Mkuu wa CCM Jijini Dodoma

MWENYEKITI wa CCM Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi MheDk. Ali Mohamed Shein na Viongozi wengine wakiwa katika meza kuu wamesimama baada ya kuwasili kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa
WAKE wa Viongozi  wakiwa wamesimama wakati Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (hayupo pichani) akiwasili katika ukumbi wa  Jakaya Kikwete Jijini Dodoma  katika Mkutano Mkuu wa CCM  uliofanyika leo 11/7/2020
WAZIRI Wakuu wastaaf wakiwa katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma wakihudhuria Mkutano Mkuu wa  CCM, wakiwa wamesimama wakati wa kuwasili kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli. (hayupo pichani) 
Waliokuwa Watia Nia kugombea Urais wa Zanzibar wakiwa wamesimama wakati wa kuwasili Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Magufuli katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi wakishangilia wakati wa kuwasili kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli (hayupo pichani)
Wageni waalikwa kutoka Vyama vya Siasa rafiki wakihudhuria hafla ya Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma. wakati Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe. John Pombe Magufili (hayupo pichani) wakiwa wamesimama.
Wasanii wa Kikundi cha TOT wakiongozwa na Msanii Bi. Khadija Kopa wakitowa burudani wakati Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Dkt. John Magufuli (hayupo pichani) akiwasili  katika ukumbi wa mkutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.