Na Jaala Makame Haji --- ZEC
Tume
ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC imeendelea na kazi ya ugawaji wa vitambulisho vya
kupigia katika vituo 272 vilivyotumika katika kazi ya Uandikishaji wa Wapiga
Kura Wapya na uhakiki wa taarifa za Wapiga Kura kwa maeneo mbali mbali ya
Unguja.
Kazi
hiyo inafanyika kwa siku mbili katika kila kituo baada kwa Wilaya zote za
Unguja ambapo awali ilifanyika katika vituo 135 vya Wilaya ya Pemba tarehe 18
hadi 19 mwezi huu.
Wakizungumza
baadhi ya Wapiga Kura waliofika vituoni kwa lengo la kuchukua vitambulisho vyao
vya kupigia kura walisema kazi inaendelea vizuri kutokana na utaratibu mzuri wa
ulioandaliwa na Tume katika ugawaji wa vitambulisho hivyo.
Walisema
kuwa, utayari wa wapiga kura kufika vituoni kuchukua vitambulisho vyao unatokana
na juhudi zinazochukuliwa na Tume pamoja na upatikanaji wa taarifa sahihi
kupitia vyombo vya habari.
Walifafanua
kuwa, ZEC kabla ya kazi hii, ilitoa elimu ya Wapiga Kura kupitia redio, TV na
mitandao ya kijamii ambapo walisambaza namba za kupiga kupitia mtandao wa
Zantel ambazo ziliwasaidia Wapiga Kura kujua vituo ambavyo vitambulisho vyao
vinapatikana pamoja na kujua namba ya box la kitambulisho.
Mkurugenzi
Baraza la Manispaa Wilaya ya Magharib “A” AMOUR ALI MUSSA ambaye ni miongoni
mwa Wapiga Kura waliofika vituoni kuchukua kitambulisho hich ameeleza kuridhika
kwake na mwenendo na utaratibu wa ugawaji wa vitambulisho ambapo ametoa wito
kwa Wananchi kujitokeza kwa wingi kuchukukua vitambulisho ambavyo vitawawezesha
kupiga kura na kuchakua viongozi wanaowataka.
No comments:
Post a Comment