Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akikagua bustani ya kabeji wakati alipotembelea banda la Jeshi la Magereza katika Kilele cha Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima Nane Nane kwenye uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu,
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu kifaa kinachotumika kutambua aina ya dawa za kulevya alizotumia mtu kutoka kwa Mfamasia wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Samwel Mbesere (kulia) wakati alipotembelea banda la mamlaka hiyo katika Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima Nane Nane kwenye uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu, Agosti 8, 2020. Wa pili kushoto ni Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, James Kaji.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuhudia wakati George Eliasi alipokuwa akisafisha mkonge kwa kutumia mashine iliyotengezwa Kishapu na mbunifu Daudi Magili (hayupo pichani) wakati alipotembelea Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima Nane Nane kwenye uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu, Agosti 8, 2020. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bibi Zainab Telack.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mashine ya kubana singa za mkonge (Pressing Mashine) wakati alipotembelea Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima Nane Nane kwenye uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu, Agosti 8, 2020. Mashine hiyo imetengenezwa Kishapu na mbunifu Daudi Magili.
No comments:
Post a Comment