Habari za Punde


Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi amezindua mtambo wa kuzima moto wenye gharama ya milioni 779.3 ulionunuliwa kutoka kikosi cha Nyumbu/SUMA JKT kwa ajili ya kuzimia moto katika shamba la miti la Sao hill ambo limekuwa likibeba uchumi wa wilaya ya Mufindi
Huo ndio mtambo wenyewe wa kuzimia moto katika shamba la Sao Hill aliouzindua Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi
Huo ndio mtambo wenyewe wa kuzimia moto katika shamba la Sao Hill aliouzindua Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi
Huo ndio mtambo wenyewe wa kuzimia moto katika shamba la Sao Hill aliouzindua Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi ukiwa unauwezo wa kurusha maji zaidi ya mita mia moja.

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.                                                                                                               

Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi amezindua mtambo wa kuzima moto wenye gharama ya milioni 779.3 ulionunuliwa kutoka kikosi cha Nyumbu/SUMA JKT kwa ajili ya kuzimia moto katika shamba la miti la Sao hill ambo limekuwa likibeba uchumi wa wilaya ya Mufindi

Akizungumza kabla ya uzinduzi wa mtambo huu Mhifadhi mkuu wa shamba la miti Sao hill Juma Mwita alisema kuwa lengo la kununua mtambo huu ilikuwa ni kuhakikisha wanaendelea kupambana na majanga ya moto ambayo yamekuwa yanatokea mara kwa mara na kuleta athari kwa serikali.

Mwita alisema kuwa shamba la miti la Sao Hill lina umuhimu mkubwa kiuchumi,kijamii na kimazingira kwa taifa la Tanzania na duniani kwa ujumla kutokana na namna shamba lilivyo hifadhiwa.

“Shamba hili ni kichecheo kikubwa cha ujenzi wa uchumi wa viwanda kutokana na kuwa chanzo cha malighafi ya viwanda vikubwa,vya kati na vidogo ambavyo hutengeneza bidhaa mbalimbali zinazotokana na mazao ya misitu” alisema  

Aliongeza kuwa kuwa TFS kwa kushirikiana na wadau wengine na uongozi wa wilaya utaendelea kujipanga kikamilifu ili kuhakikisha majanga ya moto yanadhibitiwa katika shamba la miti la Sao Hill.

Mwita alisema kuwa wamekuwa wakitoa elimu na vifaa vya kuzimia moto kwa wananchi wanaolizunguka shamba hilo mara kwa mara kwa lengo la kuendelea kuwakumbusha madhara yanayotokana na moto katika shamba hilo.

Akizungumza mara baada ya kuzindua mtambo huo wa kuzimia moto Mkuu wa mkoa huyo aliwapoongeza TFS kwa mchango wao kiasi bilioni tano kama sehehemu ya mchango wao kwa jamiii kwa kipindi cha awamu ya utawala wa serikali ya awamu ya tano

Licha ya kuwapongeza Hapi aliwataka wafanyazi wa shamba hilo kuwajibika na kutimiza wajibu kwenye majukumu ambayo wamepangiwa kuyatumikia kwa lengo la kuleta maendeleo ya taifa na kukuza uchumi wa wananchi kwa ujumla

Hapi aliwataka viongozi wa TFS waliopo katika shamba la miti la Sao Hill kuhakikisha wanautunza vilivyo mtambo huo wa kuzimia moto kwa kuwa umekuwa wakisasa zaidi na unauwezo wa kusaidia kuzima moto katika maeneo mbalimbali ya wilaya hata mkoa pale inapohitajika.

Aliwaomba wananchi kuacha mara moja tabia ya kuchoma moto kwenye mashamba ya miti kwa kuwa kufanya hivyo kunarudisha nyuma maendeleo kwa kufifisha juhudi za kukuza uchumi wa taifa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.