Habari za Punde

WAZIRI MKUU AKAGUA MIRADI YA UJENZI WA BWAWA LA KUZALISHA UMEME WA MAJI LA JNHPP NA MRADI WA KITUOCHA RELI YA KISASA MOROGORO

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha reli ya kisasa Morogoro, ambapo mpaka Novemba 15, 2020 ujenzi wa kipande cha Dar es Salaam mpaka Morogoro utakua umefikia asilimia 90, Mkoani Morogoro, leo Novemba 18, 2020
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha reli ya kisasa, mkoani Morogoro ambapo aliwasisitiza umuhimu wa kutumia fursa ya ujenzi wa mradi huo ili waweze kujiletea maendeleo,
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha reli ya kisasa Morogoro, ambapo mpaka Novemba 15, 2020 ujenzi wa kipande cha Dar es Salaam mpaka Morogoro utakua umefikia asilimia 90, Mkoani Morogoro, leo
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipewa maelezo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa juu ya maendeleo ya ujenzi wa kituo cha reli ya kisasa, mkoani Morogoro,
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia sehemu ya ujenzi wa mradi wa Kuzalisha Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), ambapo alishuhudia tukio la uchepushaji wa maji ya mto Rufiji kwenye handaki ili kupisha ujenzi wa tuta kuu la bwawa la kufua umeme mkoani Pwani, 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nyumba wa Misri, Dkt. Asim Abdelhamid Hafiz, mara baada ya kuzindua  uchepushaji wa maji ya mto Rufiji kwenye handaki ili kupisha ujenzi wa tuta kuu la bwawa la kufua umeme mkoani Pwani,
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa uchepushaji maji ya mto Rufiji kwenye handaki ili kupisha ujenzi wa tuta kuu la bwawa la kufua umeme mkoani Pwani, leo Novemba 18, 2020.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.