Habari za Punde

Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar yataka Wakandarasi wa ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Makunduchi kumaliza kwa wakati

 Na Maulid Yussuf WEMA

Mkoa wa Kusini Unguja.

Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar  imeitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kuwasimamia Wakandarasi wa ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Makunduchi ili kuhakikisha kinamalizika kwa wakati.

Imesema Muonekano wa hali ya ujenzi unavyoedelea hivi sasa  haujaridhisha kumalizika ukilinganisha na makubaliano ya muda  wa makabidhiano waloekeana.

Akizungumza wakati walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho Mhandisi Khamis Adam Khamis amesema awapi ujenzi huo walikubaliana kimalizika November2019 lakni kutokana na changamoto ya korona  ujenzi huo hawakuweza kumaliza.

Aidha amefahamisha kuwa kutokana na makubaliano ya hatua nyengine  walitarajia kukabidhiana Disember 31 mwaka Huu, lakini amesema ni  jambo linalotia hofu kukabidhiwa  kwani hali ya ujenzi unavyoonekana kumaliza kwake bado ni changamoto.

Aidha Mwenyekiti hiyo amewashauri vijana wa mkoa wa kuaini kujitokeza kusoma katika hicho kupitia fani mbalimbali kwa lengo la kujiajiri badala ya kukaaa na kisubiri ajira kutoka Serikalini.

Amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imekuwa ikifanya kila jitihada kuhakikisha inaanzisha vyuo mbalimbali vikiwemo vya Mafunzo ya Amali ili kuwasadia vijana  na kuwawezesha kusoma na kujiajiri kwani imeonekana  ajira ndio changamoto kubwa duniani kote na sio Zanzibar pekee.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa mamalaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar Dkt. Bakari Ali Silima amesema  Mkandarasi akiweka bidii na kuongeza nguvu kazi basi kuna uwezekano wa kazi hiyo  kukamilika ndani ya muda ulio takiwa, lakini kwa kasi ilivyo sasa bado haijaridhisha.

Pia Mkurugenzi huyo amesema licha ya kutokamilika kwa jengo hilo lakini bado kutakuwa na changamoto ya vifaa vya fani ya uvuvi, pamoja na zana za kilimo na ufugaji bado havijafika lakini Amesema endapo litakamilika kwa wakati chuo kitaanza kutoa Mafunzo katika fani zilizobaki.

Kwa upande wake Mhandisi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar ndugu Salum Ali Juma amesema  kutoweza kukamilika kazi hiyo kwa wakati kunasababishwa na kuzorota kwa utendaji wa kazi wa mkadarasi wa ujenzi huo, hali iliyo pelekea kunyanganywa kwa baadhi ya kazi na kupewa mkandarasi mwengine ili kazi zipate kwenda vizuri.
 
Mshauri elekezi wa mradi wa ujenzi wa vyuo vya Amali vya Daya na Makunduchi, ndugu Mohammed Sleiman Nassor amesema  tatizo pia linasababishwa na ugumu wa fedha wa mkandarasi wa ujenzi huo ambapo wafanyakazi huwaweka kidogo kwa kubana matumizi, ingawa na kuwepo kwa changamoto ya mchanga kutopatikani vizuri .

Ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali cha Makunduchi ulianza mwaka 2016 chini ya kampuni ya ujenzi mindset company limited kutoka Tanzania Bara.

Wakati huo huo Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya vyuo ya Amali Zanzibar, imetembelea kituo cha binafsi cha Mafunzo ya Amali kiliopo Makunduchi Kigaeni na kumtaka mmiliki wa kituo chicho bw Nicolus, kuwasilisha mpango kazi wa kukiendeleza kituo hicho ndani ya wiki mbili, na akishindwa kufanya hivyo, Bodi itachukua hatua nyengine za kisheria dhidi yake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.