Habari za Punde

Shirika la huduma ya kujitolea nje ya mipaka ya Tanzania (VSO) yafanya ziara ofisi ya vijana Zanzibar

Mwenyekiti wa Vijana Zanzibar Khamis Rashid Kheir (Makoti) akimkaribisha Mkurugenzi wa  V.S.O Down Hoyle pamoja na watendaji wake katika Ofisi za Baraza la  Vijana Mwanakwerekwe Zanzibar.


Mwenyekiti wa Vijana Zanzibar Khamis Rashid Kheir (Makoti) akimkaribisha Mkurugenzi wa  V.S.O Down Hoyle pamoja na watendaji wake katika Ofisi za Baraza la  Vijana Mwanakwerekwe Zanzibar.


Program Maneja Elimu na Vijana (VSO) Bonavita Eahaihi akizungumza na watendaji wa Baraza la Vijana mambo mbalimbali ya kujiendeleza huko Ukumbi wa Baraza la Vijana Mwanakwerekwe Zanzibar.
Mkurugenzi wa  V.S.O Down Hoyle akizungumza na watendaji wa Baraza la Vijana mambo mbalimbali ya kujiendeleza huko Ukumbi wa Baraza la Vijana Mwanakwerekwe Zanzibar.
Watendaji wa Baraza la Vijana wakiwa katika Picha ya pamoja na Watendaji wa (VSO) Tanzania mara baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika  Ukumbi wa Baraza la Vijana Mwanakwerekwe Zanzibar.
Mkurugenzi wa  V.S.O Down Hoyle (kulia )akitoa maelekezo kwa watendaji wa kituo cha ushoni kilicho chini ya Baraza la Vijana Wilaya ya Magharibi B huko Kwamchina Zanzibar wa mwanzo kushoto ni Mwenyekiti Baraza la Vijana Wilaya ya Maghribi B Unguja 

Program Maneja Elimu na Vijana (VSO) Bonavita Eahaihi (katikati) akiwashauri Watendaji wa Green House (hawamo pichani) kuzalisha bidhaa zenye ubora huko Fuoni Kibondeni Zanzibar.


Mratibu Baraza la Vijana Wilaya ya kati akitoa maelekezo kwa Watendaji wa VSO  kuhusu uendeshwaji wa radio jamii (Kati FM Radio) iliyopo Binguni Wilaya ya Kati Zanzibar.

PICHA NA FAUZIA MUSSA / MAELEZO ZANZIBAR 

Na Sabiha Khamis   Maelezo      05/06/2020

Mkurugenzi wa Shirika la Huduma ya Kujitolea Nje ya Mipaka Tanzania (VSO) Dawn Hoyle amewataka vijana kutumia fursa zilizopo katika mazingira yao yaliowazunguka ili kuepuka kuwa wategemezi bali watumie ujuzi walionao katika kufikia malengo waliojiwekea.

Ameyasema hayo wakati akifanya ziara ya kuvitembelea vituo mbali mbali vya ujasiriamali ambayo ilianzia katika kituo cha ushoni na shamba la Green House la Vijana liliopo Fuoni Kibondeni Wilaya ya Magharibi “B” na kumalizia katika kituo cha Redio jamii Kati Fm iliopo Wilaya ya Kati.

 Amesema vijana wanapaswa kutumia ujuzi na vifaa walivyovipata ili kuweza kutengeneza fedha zitakazoweza kusaidia kuendesha miradi na kukuza mitaji pamoja na kukidhi mahitaji yao.

“Ingawa kuna uhaba wa eneo la kufanyia kazi lakini tunapaswa kutumia ujuzi na vifaa tulivyonavyo katika kufikia malengo”

Vile vile aliwataka vijana wa Shamba la Green House kushirikiana na vikundi vya wakulima katika kujitengenezea soko la uhakika ambalo litasaidia kuuza mazao yao kwa urahisi na kujipatia faida itakayoendana na bidhaa hizo.

“Ni vyema tukashirikiana na wakulima pamoja na mahoteli ili kupata soko la uhakika katika kuuza bidhaa zetu”

Kwa upande wake Afisa Mipango wa Elimu na Vijana kutoka Shirika la Huduma ya Kujitolea Nje ya Mipaka Tanzania Bonavitita Eahaihi amesema amefurahi kuona kazi mbali mbali zinazofanywa na vijana ambao wameweza kusimamia miradi yao wenyewe na kuongeza chachu ya maendeleo katika jamii.

Hata hivyo amesema mbali na changamoto zinazowakabili ikiwemo uhaba wa fedha za kuendesha miradi  na ujuzi wanapaswa kutumia fursa zilizopo ili waweze  kupanua wigo wa kazi zao.

 Aidha aliwataka kutumia nafasi walizonazo kuuza bidhaa ambazo wanazitengeneza kupitia kituo cha ushoni pamoja na kutumia redio kuuza vipindi mbali mbali ambazo zitasaidia kupata kiwango kikubwa cha fedha zitakazosaidia kupanua kazi wanazozifanya.

Vile vile aliwataka kuendelea kushirikiana na vijana wengine na wadau mbali mbali bila ya kuiacha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambao ndio wadau wakubwa wamefanya mengi kwa vijana waendelee kutanua kazi zao na kutatua changamoto walizonazo.

Pia alimshukuru Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar Khamis Rashid Kheir kwa kushirikiana na Vijana katika kutengeneza miradi na ajira nyingi kwa vijana ili kuweza kufikia malengo.

Nae Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Wilaya ya Magharibi “B” Hassan Ali Nassor amesema lengo la ziara hiyo kuwashajihisha na kuwapa moyo vijana kupitia kazi wanazozifanya na kutumia fursa ili kujiajiri pia amewashukuru washirika wa shirika hilo kwa kuwaunga mkono vijana katika kazi zao.

Maadhimisho ya watu wanaojitolea yatafanyika tarehe 05/12/2020 ambayo yatafanyika Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja


 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.