Habari za Punde

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali akutana na mwakilishi wa mtandao wa Elimu MINDZU


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said ( kushoto ) akizungumza na Mwakilishi wa Mtandao wa Elimu MINDZU, Ndg. Khalaf Rashid, ofisini kwake Mazizini Mjini Unguja, juu ya namna ya kuanza kufundisha kwa kupitia mtandao kwa wanafunzi wa kidatu cha kwanza mpaka cha nne kwa masomo ya sayansi hapa nchini.
Picha na  Maulid Yussuf WEMA

Na Maulid Yussuf WEMA

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said amefanya mazungumzo na Mwakilishi wa mtandao wa Elimu MINDZU Mr Khalaf Rashid.

Mazungumzo hayo yamefanyika ofisini kwake mazizini Mjini Unguja yakiwa na lengo la kuangalia uwezekano wa kuanzisha kusomesha kwa njia ya mtandao kwa masomo ya sayansi kuanzia kidatu cha kwanza hadi cha nne hapa nchini.

Mhe Simai amesema njia hizo tayari zimeshaanza kutumika katika mbalimbali maarufu hasa katika bara  la Asia na kwengineko duniani.

Amesema wanatarajia kuanza kutumika katika simu na TV maalum ya Serikali pamoja kutokana na Wanafunzi kutoruhusiwa cm wanapokuwa Skuli, ambapo masomo yatawekwa kwa mfumo maalum wa kila darasa ili kuwapa uzoefu wanafunzi wa kusoma kupitia mitanadaoni na sio maktaba pekee.

Mhe Simai amefahamisha kuwa kuwepo kwa njia hiyo ya kufundisha kupitia mtandao kunaweka kumbukumbu ya wakati wa nripuko wa maradhi ya COVID 19, ambapo Wizara ilifanikiwa kutoa elimu kupitia njia za mitandaoni.

Hivyo, Mhe Simai ameahid kuliendeleza suala hilo pamoja na kuwepo changamoto ya kifedha katika Serikali na Wizara lakini washirikiana na wadau mbalimbali ili kusaidia mipango kama hiyo kwa lengo la kukuza sekta ya Elimu nchini.

Aidha Mhe Simai amesema suala hilo ni miongoni mwa ubunifu aliouanzisha katika kutekeleza maagizo ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi la kuwataka Mawaziri wake kuwa wabunifu katika utendaji wa mjukumu yao.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mtandao wa Elimu MINDZU, Mr Khalaf Rashid amesema ameamua kufanya hivyo kwa lengo la kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kukuza uchumi wake kwa kutanua wigo kupitia sekta ya Elimu hapa nchini.

Amesema kufanikiwa kwa mtandao huo wa Elimu kutasaidia kutia kwa teknolojia ya Elimu kwa kuongeza ubira wa Elimu kwa faida ya kizazi kiliopo na cha baadae.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.