Habari za Punde

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango atembelea Makao Makuu ya ZSSF Kilimani

Meneja wa Huduma za Wateja, Nd Khamis Thani akimkabidhi Mh Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe Jamal Kassim kadi yake mpya ya uanachamabaada ya kujiunga na mfuko wa kijamii.

Nd Omar Nassibu akimhudumia Mh Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe Jamal Kassim  kwa kumuwekea sawa taarifa, kumpiga picha, na kuchukua alama zake za vidole.

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe Jamal Kassim akiendesha kikao cha Kazi baina yake Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko na Menejimenti ya Mfuko huko katika Makao Makuu ya ZSSF Kilimani
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe Jamal Kassim  akikagua mafaili ya wanachama wanao subiri malipo ya mafao na kutaka Mfuko kuharakiza miamala yake ili wanachama wapate huduma haraka wakati alipofika katika Makao Makuu ya ZSSF Kilimani
Mkurugenzi Muendeshaji wa ZSSF, Sabra Machano akitoa ufafanuzi wa huduma ya usajili, na  Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe Jamal Kassim ameutaka Uongozi uifanye huduma hii kwa kutumia mitandao na mifumo kumpunguzia usumbufu mwanachama.



  Bi Mwanajuma Waziri alimpoke Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe Jamasl Kassim na kumfahamisha tunatoa vipi huduma kwa wateja wakati alipofanya ziara katika Makao Makuu ya ZSSF Kilimani

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.