Habari za Punde

Day Care Centre Zaagizwa Kuwa na Wataalam wa Malezi kwa Watoto.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya-Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akitoa kwa zawadi kwa Magreth Peter mwanafunzi bora katika Mahafali ya tatu ya Tasisi ya Ustawi wa Jamii Kampasi ya Kisangara Mkoani Kilimanjaro.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya-Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akizungumza wakati wa Mahafali ya Tatu ya Tasisi ya Ustawi wa Jamii Kampasi ya Kisangara yaliyofanyika leo Mkoani Kilimanjaro.
Wahitimu wa Astashahada na Stashahada za Ustawi wa Jamii Taasisi ya Ustawi wa Jamii Kampasi ya Kisangara wakiwa katika Maandamano ya kitaaluma ya Mahafali ya Tatu ya Kampasi hiyo yaliyofanyika Leo Mkoani Kilimanjaro.

Baadhi ya Wahitimu wa Astashahada na Stashahada za Ustawi wa Jamii kutoka Taasisi ya Ustawi wa Jamii Kampasi ya Kisangara Mkoani Kilimanjaro katika mahafali ya tatu ya Kampasi hiyo.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

 Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro

Wamiliki wa Vituo vya Malezi kwa Watoto (Day Care Centre wamewatakia kuwa na watalaam wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ili kutoa Malezi sahihi kwa watoto wanaowahudumia katika vituo hivyo. 

 

Agizo hilo limetolewa na Dkt. John Jingu wakati akiwatunuku Stashahada na Astashahada kwa wanafunzi 156 wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Kampasi ya Kisangara Mkoani Kilimanjaro. 

 

Amesema kuwa hakuna taifa ambalo litaendelea vizuri kama Msingi wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto hautochukuliwa kwa umuhimu unaostahili. 

 

Ameongeza kuwa kwa kipindi hiki jamii imekuwa ikishirikina na Serikali katika kuanzishwa na Kujenga Vituo vya Malezi na Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto katika ngazi ya Jamii vitakavyosaidia kulea watoto katika maeneo husika.

 

Amesisitiza kuwa mafunzo ya Elimu ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto yanayotolewa na Taasisi ya Ustawi wa Jamii Kijitonyama Kampasi ya Kisangara yamekuwa ni Msingi sana hasa katika Ustawi wa Watoto na familia nchini.

 

" Sasa ili suala hili lifanikiwe tufanye haraka kumaliza mitaala ya Mafunzo ya Elimu ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ili mafunzo haya yaendelee kutolewa kwa vile kuna uhitaji mkubwa wa masomo haya " alisema

 

Aidha Dkt. Jingu ameiagiza Menejimenti ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii kuendelea na uwekezaji katika rasilimali watu katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii Kampasi ya Kisangara ili iwe mahiri katika utoaji wa mafunzo ya malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto nchini.

 

Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt. Joyce Nyoni ameishukuru Serikali kwa kuendelea kusimamia Taasisi ya Ustawi wa Jamii kwa kutoa miongozo na maelekezo mbalimbali yenye lengo la kuhakikisha fani ya Ustawi wa Jamii inaleta matokeo chanya katika jamii.

 

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Vickness Mayao akizungumza kwa niaba ya Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt Naftali Ng'ondi amesema Idara ya Ustawi wa Jamii itaendelea kusimamia Taasisi ya Ustawi wa Jamii Kampasi ya Kisangara ili iweze kutoa mafunzo yatakayosaidia jamii kubadilika na kuendelea.

 

Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara kilianza Mwaka 1986 kwa kutoa mafunzo ya Elimu ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto na mwaka 2020 kilikabidhiwa rasmi katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii Kijitonyama.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.