KATIBU wa Mbunge wa Jimbo la Mkoani Mariam Said
Khamis (kulia) akimkabidhi mita 50 za mpira wa maji, Mwenyekiti wa bonde la
Darajani Makombeni Nassor Hakim Haji, uliotolewa na Mbunge wa jimbo hilo
Profesa Makame Mbarawa Mnyaa ikiwa ni ahadi yake kwa wakulima hao.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MAFUNDI kutoka Mamlaka ya Maji Zanzibar ofisi ya
Pemba (ZAWA), wakiteremsha mchikichi(mashine ya maji)ndani ya kisima pamoja na
mpira wake wa kutolea maji, kwa ajili ya umwagiliaji wa bonde la Kindani
Darajani Makombeni, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya mbunge wa jimbo la Mkoani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
WANANCHI wakinawa mikono baada ya kumalizika kazi ya
usafishaji wa kisima cha maji pamoja na uwekaji wa mpira mpya mita 50 ndani ya
kisima hicho, ili wakulima wa mpunga bonde la Kindani Darajani makombeni waweze
kutumia katika umwagiliaji.(PICHA NA
ABDI SULEIMAN, PEMBA)
BAADHI ya mashamba ya mpunga ya umwagiliaji maji
katika bonde la Kindani Darajani Makombeni, wakisubiri maji baada ya
kulitaayarisha shamba kwa ajili ya kilimo cha awamu ya pili cha mpunga.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
No comments:
Post a Comment