Habari za Punde

Rais Mstaafu Dk Shein mgeni rasmi Ufunguzi wa vituo vya ubunifu wa kisayansi Uroa

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Idrissa Muslim Hija akitoa maelezo ya kitaalamu ya Kituo cha Ubunifu wa Kisayansi kwa niaba ya Vituo 22 vya Unguja na Pemba   hafla iliyofanyika Uroa Mkoa wa Kusini Unguja.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Simai Mohammed Saidi akisisitiza umuhimu wa kuvitunza vituo vya Ubunifu wa Kisayansi wakati wa Ufunguzi Uroa  Wilaya ya Kati ikiwa ni Miongoni mwa Shamrashamra za miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.


Rais Mstaafu wa awamu ya saba wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein akizungumza machache baada ya kuzindua School Hub ya Uroa Wilaya ya Kati Unguja

Picha na Maryam Kidiko / Maelezo Zanzibar
 

Na Miza Kona / Maelezo Zanzibar     09/01/2021

Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar awamu ya saba Dk. Ali Mohamed Shein amesema Mapinduzi ya mwaka 1964 yamekuja kumkomboa mnyonge kutoka katika ubaguzi na kuweza kujitawala .  

Dk. Shein ameyasema hayo huko Uroa Wilaya ya Kati Unguja wakati wa ufunguzi wa kituo cha Ubunufu wa Kisayansi kwa niaba ya vituo 21 vilivyojengwa ikiwa ni shamra shamra ya maadhimisho ya kutimiza miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema Mapinduzi yameleta umoja, mashirikiano, mshikamano, maridhiano na mapenzi kwa wazanzibari na kuweza kjitawala wenyewe na kupata huduma zote muhimu za kijamii ikiwemo elimu ambayo ni mkombozi wa maendeleo.

“Mapinduzi yameleta mambo muhimu ya msingi ikiwemo elimu na afya ambapo hapo awali ilikuwa ikitolewa kwa ubaguzi na wananchi waliowanyonge hawakupata fursa hiyo kwani nafasi hizo walinufaika mabepar”, alieleza Dk Shein.

Dk. Shein ameeleza elimu ya sayansi ni kichocheo kikubwa cha kuleta maendeleo nchini hivyo amewata wazazi na walimu kuwashajihisha wanafunzi kujikita kusoma masomo ya sayansi ili kukuza kiwango cha elimu kwa kuleta maendeleo na kupata wataalamu wazuri.

Amefahamisha kuwa nchi nyingi duniani zimekuwa zikiwasomesha vijana wake masomo ya sayansi ili kuboresha elimu na kupata vijana wenye taaluma mbali mbali nchini kwa lengo kupata ufanisi zaidi.

Dk. Shein amesisitiza kuvitumia na kuvitunza vituo hivyo ili viweze kudumu na kuweza kupata wataalamu na kuongeza ufanisi kwa vjiana katika masomo ya sayansi

Nae Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Simai Mohamed Said amesema vituo hivyo vitawasaidia vijana kutumia ubunufu wao na ujuzi waliokuwa nao katika kujifunza zaidi na kuweza kujipatia ajira kupitia utaalamu walionao.

Akitoa taarifa ya kitaalamu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Idrisa Muslim Hija amesema mradi huo una lengo la kuimarisha ubora wa elimu katika masomo ya sayansi na Hisabati kwa ngazi elimu ya sekondari na kiingereza kwa elimu ya msingi.

Aidha amefahamisha kuwa pia utainua ubora wa elimu Zanzibar hasa katika kuongeza ufaulu kwa wanafunzi na kuimarisha usomeshaji katika masomo ya sayansi, hisabati na lugha ya kiingereza.

Mradi huo wa miaka mitano 5 umejengwa kupitia mradi wa Zanzibar Improving Student (ZIPS) ambao umefadhiliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mkopo wa Benk ya Dunia na umegharimu Dola za Kimarekani milioni 35 hadi kumalizika kwake.   

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.