Habari za Punde

TFF yakiri kuwepo mapungufu katika kuendesha klabu za soka

 NA MWAJUMA JUMA

SHIRIKISHO la Soka Tanzania TFF limekiri kuwepo na upungufu mkubwa wa uwendeshaji katika eneo la Utawala bora kwa klabu.

Hayo yameelezwa na Rais wa Shirikisho hilo Wares Karia alipokuwa akifunguwa Mafunzo ya Utawala bora kwa wenyeviti wa klabu za soka Tanzania Bara uliofanyika visiwani hapa.

Alisema kuwa Shirikisho lao linefanikiwa katika wanachama wao wa mikoa kwenye eneo hilo lakini kwa upande wa klabu bado ni tatizo.

Alifahamisha kwamba katika klabu ni lazima kuwepo mgawanyiko wa majukumu na sio kufanya mtu mmoja.

Alisema kuwa utakuta katika klabu kuna mtu mmoja ambae ndie yeye anaefanya majukumu yote huku akisahau kuwa Kila kiongozi akiwa anafahamu kuwa atekeleze majukumu yake.

"Haiwezekani kuona katika klabu mtu mmoja huyo ndie anakuwa anatekeleza kila kitu ni lazima tuwe na mgawanyo wa madaraka", alisema.

Aidha  alieleza kuwa pamoja na kuwa wamekuwa wakitoa Mafunzo mbali mbali ya kuhusu uongozi lakini viongozi ambao wanapatikana  ni hao hao na ndio maana Kila kitu kinafanywa na yeye.

Hata hivyo alishukuru kwa kuwapata wahusika zaidi wa Mafunzo hayo ambao watakapoondoka hapa watakuwa na uwelewa mkubwa juu ya dhana ya Utawala bora.

Mapema Makamo wa Rais wa Shirikisho la Soka Zanzibar ZFF Salum Ubwa aliwaomba viongozi wa TFF kuwasimamia vyema ili na wao waweze kuwa Shirikisho kubwa Kama lilivyo la kwao.

Alisema Zanzibar na wao wanataka wawe na Shirikisho kubwa lakini wanashindwa kuona wanafikia jambo ambalo wanatakiwa kusaidiwa.

Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na TFF yanalengo la kiwajengea uwezo kwenye eneo la Utawala bora yanafanyika kwa siku mbili ambapo jana washiriki ni viongozi wa klabu za ligi kuu Tanzania Bara na leo Januari 24 watashiriki viongozi wa klabu za soka za ligi kuu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.