Habari za Punde

Wajumbe wa Jumuiya Rafiki ya Wanawake na Watoto yawapiga Msasa Wajumbe wake wa kujitolea

 Na Takdir Suweid, Wilaya ya Magharibi ‘’B’’.                                     03-01-2021.

 

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Magharibi  Tauhida Gallos Nyimbo amesema amewataka Wajumbe wa Jumuiya Rafiki ya Wanawake na Watoto RAWWAZA na Taasisi nyengine zinazofanya kazi na jamii kuzingatia maadili ili kuweza kuleta mabadiliko katika Taifa.

 

Amesema malengo ya jumuiya hizo ni kuisaidia jamii katika Nyanja mbali mbali ikiwemo kuwasaidia kuacha kujishirikisha na vitendo viovu,kuwajenga kimaadili na uadilifu ili waweze kuwa Raia wema wa hapo baadae hivyo ni vyema kujiepusha na Tabia zisizokubalika katika jamii ili kuweza kuwa kioo kwa jamii husika.

 

Akifunguwa mafunzo elekezi kwa Wajumbe wa kujitolea katika Jumuiya hiyo,yalioandaliwa na Jumuiya ya Rawwaza huko katika Ukumbi wa Baraza la Manispaa Wilaya ya Magharibi A amesema lengo la kutoa elimu hiyo ni kuwafanya waendane na maadili na miiko ya Jumuiya hiyo.

 

 

Aidha amewasisitiza Wajumbe hao wa kujitolea kuwa Msatari wa mbela katika kuwatetea,kuwaonesha njia sahihi watoto wa kike ili waweze kujikinga na kukataa kushiriki katika matendo yatakaowaharibia malengo na ndoto za maisha yao.

 

Aliwasilisha mada katika mafunzo hayo Katibu wa Jumuiya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar Tatu Hussein Abdallah kuzingatia miongozo iliowekwa na Jumuiya hiyo ili kuweza kupata fursa zilizopo bila usumbufu.

 

Nao Washiriki wa Mafunzo hayo wameahidi kushirikiana ili kuweza kufikia malengo ya kuisaidia Serikali katika kuwashugulikia Wanawake wajane,Watoto yatima,Wenye ulemavu na Wazee katika maeneo ya Mjini na Vijijini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.