Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi ajumuika na wananchi katika maziko ya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad , Nyali Mtambwe Pemba

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, wakati wa maziko yake yalifanyika Kijijini kwao Nyali Mtambwe Wilaya ya Wete Pemba.
RAIS wa Zanzibar Mstaaf Awamu wa Sita Alhajj Dk. Amani Karume akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, wakati wa maziko hayo yaliofanyika Kijijini kwao Nyali Mtambwe Wilaya ya Wete Pemba.
RAIS Mstaaf wa Zanzibar Awamu ya Saba Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad katika maziko yaliofanyika Kijijini kwao Nyali Mtambwe Wilaya ya Wete Pemba.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad katika maziko yaliofanyika Kijijini kwao Nyali Mtambwe Wilaya ya Wete Pemba,.
WANAFAMILIA ya Marehemu aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad wakiweka udongo katika kaburi wakati wa maziko hayo yaliofanyika Kijijini kwao Nyali Mtambwe Wilaya ya Wete Pemba
VIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo wakiongozwa na Mlezi wa Chama hicho Mhe. Zitto Kabwe wakiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, wakati wa maziko yake yaliofanyika Kijijini kwao Nyali Mtambwe Wiliya ya Wete Pemba.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Khalid Ali Mfaume.(hayupo pichani) baada ya kumalizika kwa maziko ya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na (kushoto kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, Rais Mstaaf wa Zanzibar Awamu ya Saba Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein na Mlezi wa Chama cha ACT-Wazalendo Mhe. Zitto Kabwe na ( kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, wakiitikia dua.
WAZIRI wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais,Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Dkt.Khalid Salum Mohammed akisomwa wasifu wa Marehemu aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, wakati wa hafla ya maziko yake yaliofanyika Kijijini kwao Nyali Mtambwe Wilaya ya Wete Pemba.
MLEZI wa Chama cha ACT-Wazalendo Mhe.Zitto Kabwe akitowa Salamu za Chama chake wakati wa maziko ya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.Maalim Seif Sharif Hamad yaliofanyika Kijijini kwao Nyali Mtambwe Wilaya ya Wete Pemba.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza baada yua kukamilioka kwa maziko ya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad  yaliofanyika Kijijini kwao Nyali Mtambwe Wilaya ya Wete Pemba.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.