Habari za Punde

Zantel yazindua ‘Pasua Anga Ki Zantel 4G’ kuwaelimisha wateja juu ya umuhimu wa mtandao wa 4G

Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Mohammed Khamis Mussa akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Zantel ijulikanayo kama ‘Pasua Anga Ki Zantel 4G’. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uchukuzi-Wizara ya Mawasiliano Zanzibar, Dkt.Mzee Suleiman Mndewa na Zuena Ali mjasiriamali mdogo. Kampeni hiyo imelenga kuelimisha umma juu ya umuhimu wa matumizi ya mtandao wa 4G katika kujiletea maendeleo.

Kampuni ya simu ya Zantel leo Machi 16, 2021 imezindua kampeni yake mpya ijulikanayo kama ‘Pasua Anga Ki Zantel 4G’ inayolenga kuwaelimisha wateja juu ya uhumimu wa mtandao wa 4Gkatika kujiletea maendeleo.

Uzinduzi huo umefanyika leo katika viwanja vya Kisonge mjini Unguja ambapo wananchi wameweza kushiriki na kujionea ni namna gani wanaweza kutumia mtandao wa 4G kwa manufaa ya kijamii na kiuchumi.

Kabla ya uzinduzi huo, Kampuni ya Zantel iliendesha mjadala ulijadili juu ya umuhimu wa mtandao wa 4G ambao uliruka kupitia televisheni ya ZBC.Mdahalo huo ulihusisha wadau mbalimbali kutoka Serikalini pamoja na wajasiriamali.

Akizungumza wakati wa mjadala huo, Mkuu wa Zantel Zanzibar Mohammed Khamis Mussa alisema “Nia yetu ni kunaendelea kuboresha mtandao wetu ili mawasiliano yapatikane Zanzibar yote kwa kasi ya 4G kumuwezesha mtumiaji kuweza kufanya mawasiliano bora na ya haraka. Na sasa tunazindua kampeni ya PASUA ANGA ki ZANTEL 4G mahsusi ili kutoa elimu kwa umma juu ya manufaa mbalimbali ya mtandao ulioboreshwa wa Zantel 4G.”

Katika uzinduzi uliofanyika viwanja vya kisonge, ulihusisha shughuli mbalimbali ikiwamo michezo ya foosball, tebal tennis, pool table huku washindi wakiibuka na vifurushi vya intaneti ya 4G vya wiki pamoja na zawadi mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.