Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla Ameaza Ziara Kisiwani Pemba leo.

Mkuu wa Wilaya ya Micheweni. CDR.Mohammed Mussa Seif akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakati wa kukagua Miradi ya Maendeleo ndani ya Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba.

Na.Othman Khamis OMPR.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdullah amewanasihi Wananchi na Wachuuzi wa Samaki wa Kijiji cha Njuguni Jimbo la Wingwi kulitumia Soko Jipya  la Kisasa la Samaki lililojengwa na Serikali ili kukidhi mahitaji yao ya Biashara.

Alisema kitendo cha Wachuuzi wa Samaki wa Kijiji hicho kuendelea kuuza samaki wao kando kando ya Bara bara  mbali ya kuhatarisha maisha yao lakini pia kinaweza kuleta athari ya Afyabzao kutokana na vumbi linalosababishwa na Gari zinazopita kila wakati eneo hilo.

Akiendelea na ziara yake ya Siku Tano Kisiwani Pemba kukaua Miradi ya Maendeleo na kujuwa changamoto zinazowakabili Wananchi wa Wilaya Nne akiwa Wilaya ya Micheweni kwa Siku ya Pili Mh. Hemed Suleiman alisema ujenzi wa soko hilo umezingatia  matakwa yaop ambayo wanapaswa kuyasimamia.

Alisema haipendezi hata kidogo kuona kwamba Serikali inajenga na Kuimarisha Miradi ya Maendeleo iliyobuniwa na Wananchi wenyewe akitolea mfano soko hilo na baadae Wananchi hao wakashinda kulitumia.

Aliwatoa hofu Wananchi na Wachuuzi hao wa Samaki wa Njuguni kwamba  huduma bora ndizo zinazotoa fursa kwa Mteja  kuzifuatilia mahali popote bila ya kujali umbali wa bidhaa iliyopo.

Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla alisema katika kukabiliana na changamoto inayowakabili Wananchi wa Jimbo hilo na wale wa Vijiji Jirani ameuagiza Uongozi wa Wilaya ya Micheweni kupitia Halmashauri ya Wilaya hiyo kutafuta eneo jipya litakalojengwa Soko kubwa litakalokidhi mahitaji yote kwa kuzingatia Miundombinu na Geografia halisi.

“ Wananchi wa Wingwi ni vyema wakafunuka na kuanza kulitumia Soko lao huku Serikali Kuu kupitia  Uongozi wa Wilaya na Halmashauri ya Micheweni pamoja na Viongozi wa Jimbo itabeba dhima ya kuwapatia Mafriji kwa lengo la kuhifadhi samaki wao.

Aliwahakikishia Wachuuzi hao kuwa Soko la samaki halichelewi kuzoeleka kwa kupata Wateja kutokana na hudum kuwa muhimu katika maisha bya kila siku ya Mwanaadamu.

Akizungumzia kero za huduma za Maji safi na salama, Umeme, Afya na Miundombinu ya Bara bara inayowakabili Wananchi wa Vijiji vya Mkia wa Ng’ombe na Chanja Kipange, Mh. Hemed  aliahidi kwamba huduma hizo muhimu  zitafikishwa katika maeneo yao  ili kuwaondoshea dhiki inayowakabili.

Mheshimiwa Hemed Suleiman alieleza kwamba huduma hizo zinazosaidia kuboresha maisha yao zimo ndani ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2020/2025 pamoja na Ahadi za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Hussein Ali Mwinyi alizozitoa wakati wa Kampeni za Uchaguzi.

Aliwakumbusha Wananchi hao kuendelea kuwa Walinzi wa Miradi inayoanzishwa na kuenezwa katika maeneo yao kwa vile imewekwa kwa lengo la kuwafaidisha na hutumia gharama kubwa za Fedha zinazotokana na kodi wanazotoa kila wakati.

Kuhusu Miradi ya ujasiri ambali ya Uchimbaji wa Mawe kwa ajili ya Kokoto inayofanywa na Wananchi wa Kijiji cha Mjini Wingwi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Serikali Kuu haiwezi kuruhusu uendelezaji wa Mradi huo kwa vile umeshaleta athari na kusababisha kupotea kwa maisha ya Wananchi.

Alisema katika njia ya kutafuta mbadala wa masuala ya ajira katika Kijiji hicho zipo sekta za Uvuvi na kilimo pamoja na ujasiri amali kupitia Vikundi vya Ushirika ambavyo Wanachi hao wanaweza kuvitumia katika kuendesha maisha yao.

Mheshimiwa Hemed alitoa agizo kwa Timu ya Wataalamu wa Sekta tofautri ndani ya Wilaya ya Micheweni kufanya Utafiti na kutoa Ripoti ndani ya Maiezi Mitatu kuelewa Wananchi wa Mjini Wingwi wanahitaji miradi gani ya kujikimu ili waendelee kuendesha maisha yao ya kila Siku.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alikemea vitendo vya baadhi ya Wanasiasa kuendelea kuwapotosha Wananchi waliokwisha jenga matumaini makubwa ya kupata Maendeleo ya haraka kutokana na mikakati ya Serikali iliyokwisha jitokeza kila mahali.

Mheshimiwa Hemed Suleiman aliupongeza Uongozi wa CCM Wilaya ya Micheweni kwa kusimamia vyema Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na kuushukuru Uongozi wa Serikali wa Wilaya ya Micheweni kuvuka lengo katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwenye Halmashauri yake.

Mapema akitoa Taarifa ya Utekelezaji Kazi za Maendeleo wa Wilaya ya Micheweni, kwa Mwezi Novemba  Mwaka 2020 hadi Machi 2021,  Mkuu wa Wilaya hiyo Nd.Mohd Seif  alisema Halmashauri ya Wilaya hiyo imejipangia kukusanya mapato zaidi ya shilingi Milioni 149.

Nd. Mohd alisema kutokana na ushirikiano mkubwa wa watendaji na Viongozi wake wamefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi Milioni 194 sawa na asillimia 131.6% na kuvuka lengo walilojipangia.

Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Hemed Suleiman Abdulla alipata fursa ya kulitembelea eneo la Bandari ya Micheweni lililowekwa kufungua fursa za Uwekezaji wa Wawekezaji Wazawa na Wageni chini ya usimamizi wa Rais wa Zanzibar aliyelenga kuweka mikakati Maalum ya Uwekezaji katika Kisiwa cha Pemba.

Akitoa ufafanuzi wa harakati za uimarishaji wa eneo hilo la Uwekezaji Mkuu wa Mkoa Kaskazini Pemba Bibi Salama Mbarouk Kahtibu alisema Taasisi zote zinazohusika na uhuishaji wa Miundombinu ya eneo hilo zinaendele vyema na majukumu yake.

Mh. Salama alisema Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba wamefarajika na uamuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa kulifanya eneo la Bandari ya Micheweni kuwa mahsusi kwa shughuli za Uwekezaji.

Alisema Micheweni inaonyesha wazi kwamba ni eneo miongoni mwa sehemu zitakazosaidia kuzalisha zile Ajira Laki 300,000 zilizokuwa zikizungumzwa na Rais wa Zanzibar Dr. Hussein Mwinyi.

Akitoa nasaha zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Hemed Suleiman aliwataka Wahandisi na Wasimamizi wa Taasisi zinazohusika na eneo hilo kuhakikisha kwamba maagizo yote yaliyotolewa na Rais wa Zanzibar yanatekelezwa kwa wakati muwafaka.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Jumapili anaendelea na ziara yake ya Siku Tano kwa kuitembelea Wilaya ya Wete katika siku yake ya Tatu.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akikagua Barabara inayounganisha eneo Maalum lililotengwa na Serikali kwa ajili ya Bandari ya Micheweni litakalotumika kwa shughuli za Uwekezaji.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Hemed Suleiman na ujumbe wake akilikagua Soko la Samaki liliopo katika Kijiji cha Njuguni Jimbo la Wingwi.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akikagua chem chem inayotoa huduma ya maji safi na salama katika kijiji cha Mkia wa Ng’ombe Wilaya ya Micheweni Mkoa Kaskazini Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.