Habari za Punde

SMZ Inakusudia Kuazishwa Kwa Chombo Maalum cha Zakka na Sadaka.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inakusudia kuazisha Chombo maalumu cha kuratibu shuhuli za zakka na sadaka ili kutoa fursa za kukuza uchumi wa kijamii  Zanzibar.

Kauli hiyo imetolewa na  Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar Othman Masoud Othman mara baada ya kukamilisha swala Ijumaa katika Masjid Swahaba Mtoni kidatu Unguja.

Makamu alifahamisha kuwa kuazishwa kwa Chombo hicho utaisaidia sana waislam kujitokeza kutimiza wajibu wao katika kendeleza Uislam.

“Jamii inamahitaji makubwa ya huduma hii kutokana na ufinyu wa fursa zinazotokana na waislamu wenyewe”.

Alifafanuwa Vyombo vya namna hiyo ni mihimu kwani hutoa fursa za kiuchumi ya kusaidiana baina ya watu wa madaraja tofauti.

Alieleza kwa mujibu wa dini ya Kiislamu mifumo ya zakka na sadaka katika jamii inahamasishwa sana ili kuondoa chuki baina Matajiri na masikini, walionacho na wasikuwanacho pamoja na kukuza uhusiano mwema  katika jamii husika

Alisema hivi sasa watu wengi hawatoi sadaka wala zaka kwa sababu hawa elimu nayo lakini uwepo wa chombo hicho utasaidia kuwazindua waumini na kuwahamisha umuhimu wa kutoa zakka na sadaka.

“Kuna watu hawatoa kwa sababu hawajui lakini kuna wengine wanajihisi wao hawahusiki lakini chombo hichi kitawapatia ufahamu wa nia hiyo” alisema Makamu wa kwanza wa Rais.

Akitoa ufafanuzi wa chombo hicho Makamu alisema kuwa waliazisha tangu 2007 lakini hakikutiliwa nguvu na kusisitiza kuwa sasa wamekusudia kulisimamia.

Alisema  katika kuhakikisha chombo hicho kinafanyakazi kwa manufaa ya umma lazima wapatikane watendaji ambao ni waadilifu na wenye kumcha Allah subnahanahu wataala.

“Ni wajibu wetu kama viongozi wa Serikali kuhakikisha watu wanapata haki zao kama Uislamu unavyotaka” alisema.

Alifahamisha kuwa kutoa Zakka ni wajibu kwa waimini wa kiislamu kwa hiyo kufanya tendo hilo hakuwezi kuwarudisha nyuma au kuwafukarisha katika biashara zao.

Makamu  aliwausia waislamu kudumisha umoja na kusaidiana hasa katika Mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Sambamba na hilo aliwata Waimini hao kutoa mawazo yao katika kuazisha chombo hicho ili kiwe bora zaidi kwa manufaa ya umma.

Alisema wako watu wengi pamoja nan tasisi nyingi ndani na nje ya nchi zinataka kufanya hivyo lakini kutokuwepo kwa chombo hicho kunaonekana kama kikwanzo kwao.

Pia alisema kitakaposimama chombo hicho kutaisaidia sana kuboresha Madrasa, Misikiti, waalimu wa madrsa pamoja na  masheikhe  mbali mbali.

Aidha aliwataka waislamu wasisite kuwaombea dua wazee waliotangulia aghera na hasa kumtakia duwa aliyekuwa Makamu wa kwanza wa Rais Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad.

Umma wa Kiislamu uliojitokeza kwa wingi katika msikiti huo ulionekana kuvutiwa na kuazisha chombo na kueleza kuwa ninkatika mambo yenye kheiry sana katika ulimwengu.

Issa Bakar Issa ambaye ni Imamu wa msikiti huo alisema watahakikisha kuwa azima hiyo njema yanye manufaa makubwa kwa umma imesimama.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.