Habari za Punde

DOLA ZA MAREKANI MILIONI 140 KUTUMIKA MRADI WA UMEME KATIKA MTO MARAGARASI

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba na Bi. Nnenna Nwabufo, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Kanda ya Afrika Mashariki, wakisaini   mikataba miwili ya mkopo wenye thamani ya dola za Marekani milioni 140 (takriban shilingi bilioni 323.4) kwa ajili ya kufadhili Mradi wa kufua Umeme wa Mto Malagarasi, Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba (kulia), na Bi. Nnenna Nwabufo, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Kanda ya Afrika Mashariki, wakibadilishana hati za mikataba miwili ya mkopo wenye thamani ya dola za Marekani milioni 140 (takriban shilingi bilioni 323.39) kwa ajili ya kufadhili Mradi wa kufua Umeme wa  Malagarasi, katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba na Bi. Nnenna Nwabufo, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa Kanda ya Afrika Mashariki,    wakionesha hati za mikataba ya mkopo wa dola za Marekani milioni 140 (takriban shilingi bilioni 323.39) kwa ajili ya kufadhili Mradi wa kufua Umeme wa  Malagarasi, hafla hiyo iliyofanyika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Jijini Dar es Salaam.

Ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba (wa pili kulia walioketi), wakiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa Kanda ya Afrika Mashariki, Bi. Nnenna Nwabufo (wa tatu kulia walioketi), baada ya hafla ya utiaji saini hati za mikataba ya mkopo wa dola za Marekani milioni 140 (takriban shilingi bilioni 323.39) kwa ajili ya kufadhili Mradi wa kufua Umeme wa  Malagarasi, katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Jijini Dar es Salaam.

 

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango – Dar es Salaam)


Na, Saidina Msangi na Ramadhani Kissimba, WFM, Dar es Salaam

Serikali ya Tanzania na Benki ya Maendeleo ya Afrika zimesaini mikataba miwili ya mkopo wenye thamani ya dola za Marekani milioni 140 (takriban shilingi bilioni 323.4) kwa ajili ya kufadhili Mradi wa kufua Umeme wa nguvu ya maji -  Malagarasi.  

 

Mikataba ymkopo huo wenye masharti nafuu imesainiwa Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba, kwa niaba ya Serikali na Bi. Nnenna Nwabufo, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Kanda ya Afrika Mashariki.

 

Akizungumza wakati wa kusainiwa kwa Mikataba hiyo, Bw. Tutuba alisema kuwa utekelezaji wa mradi huo utaijengea TANESCO uwezo wa usambazaji wa vifaa vya kuunganisha wateja 4,250 katika Wilaya za Kigoma, Kibondo na Kasulu ikiwemo kaya 1,000 zenye kipato cha chini, zahanati 4 na shule za msingi 6.

 

“Mradi huu utahusisha ujenzi wa kituo kipya cha uzalishaji wa umeme wa gridi ya 49.5 MW chenye uwezo wa   kuzalisha wastani wa GWh 181 za umeme kwa mwaka ili kuboresha usambazaji wa umeme na  kupunguza utegemezi wa uzalishaji wa umeme kwa kutumia mafuta mazito ”, alisema Bw. Tutuba

 

Alieleza kuwa mradi huo unatarajiwa kugharimu  takribani dola za Marekani milioni 144.1 ambapo Benki ya Maendeleo ya Afrika itatoa dola za Marekani milioni 140 na Serikali ya Tanzania itachangia dola za Marekani milioni 4.14 zilizobaki.

 

“Kati ya fedha hizo, dola za Marekani milioni 120 zitatolewa kupitia dirisha la Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) na dola za Marekani milioni 20 kupitia Africa Growing Together Fund”, alifafanua Bw. Tutuba.

 

Aidha, Bw. Tutaba alisema kuwa mradi huo utajumuisha ujenzi wa njia ya usafirishaji wa umeme, upanuzi wa mtandao wa kusambaza umeme wa 132kV na ununuzi wa transfoma mpya 15 ili kuongeza uwezo wa kusambaza wa umeme kwa wananchi.

 

Aliongeza kuwa kusainiwa kwa mikataba hiyo kutaongeza kiwango cha fedha kilichotengwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa ajili ya kufadhili miradi ya sekta ya nishati nchini Tanzania kutoka takriban dola za Marekani milioni 325.19 hadi kufikia dola za Marekani milioni 465.19 (takriban shilingi trilioni 1.07).

Aliongeza kuwa mradi huo pia ni  sehemu ya utekelezaji wa  vipaumbele vya Benki ya Benki ya Mandeleo ya Afrika vya kuongeza uwekezaji kwenye sekta ya nishati ya umeme ili kuchochea maendeleo ya viwanda na kuboresha maisha ya watu barani Afrika.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Kanda ya Afrika Mashariki Bi. Nnenna Nwabufo alisema kuwa mradi huo ni moja ya miradi sita iliyoidhinishwa na benki hiyo katika kipindi cha miaka mitatu.

 

Aliitaja miradi hiyo kuwa ni mradi wa barabara za mzunguko jijini Dodoma wenye thamani ya dola za Marekani milioni 180, Mradi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Msalato (dola 271m), barabara ya Kabingo – Kasulu – Manyovu (dola 256m), barabara ya Bagamoyo – Horohoro – Lunga – Malindi (dola 150m) na Mradi wa usambazaji umeme wa Nyakanazi – Kigoma (dola 123m)

 

B1. Nnenna alisema kuwa uwekezaji wa Benki yake nchi Tanzania imefikia thamani ya dola za Marekani bilioni 2.33 zilizowekezwa katika sekta za miundombinu ya usafiri na usafirishaji, nishati ya umeme, maji na usafi wa mazingira, kilimo, utawala bora na fedha

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.