Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla Azungumza na Balozi Mdogo wa China Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla wa Pili kutoka Kushoto akizungumza na Balozi mdogo wa China aliyepo Zanzibar Bw.Zhang Zhisheng aliyefika afisini kwake Vuga kwa ajili ya kujitambulisha na kubadilishana mawazo juu ya masula mbali mbali ya maendeleo.

Na.Kassim Salum OMPR,

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendeleza uhusiano na ushirikiano na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China ulioasisiwa tangu mwaka 1964 baada ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.

Mhe. Hemed alieleza hayo wakati akizungumza na Balozi mdogo wa China Bw.Zhang Zhisheng alifika afisini kwake Vuga kwa ajili ya kujitambulisha na kubadilishana mawazo juu ya masula mbali mbali ya maendeleo baina ya pande mbili.

Amesema Zanzibar inathamini mchango unaoendelea kutolewa na Serikali ya Jamuhuri ya watu wa China kupitia sekta tofauti ikiwemo Afya, Miundombinu pamoja na sekta nyengine za kijamii na kiuchumi.

Akizungumzia sula la uwekezaji Makamu wa Pili wa Rais amemuhakikishia Balozi mdogo wa china Bw.Zhang Zhisheng kuwa seikali ya mapinduzi Zanzibar inawakaribisha wawekezaji kutoka nchini China kuja kuekeza Zanzibar kwani mazingira yapo salama kwa ajili ya uwekezaji.

Amesema serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na Dk. Hussein Ali Mwinyi imenzisha wizara maalum inayoshughulikia Uchumi wa Buluu hivyo inawakaribisha wawekezaji wa China kuja kuekeza kwa kujenga viwanda vya Uvuvi na serikali itatoa kila aina ya ushirikiano unaohitajika.

Makamu wa Pili wa Pili wa Rais akizungumzia suala la sekta ya Afya amesema ameipongeza serikali ya Jamuhuri ya watu wa China kwa mchango na msaada wao kwa kutoa wataalamu kuja kutoa huduma Zanzibar katika Spital ya Mnazi mmoja na Spital ya Abdalla Mzee kwa Pemba.

Nae Balozi Mdogo wa China Bw. Zhang Zhisheng amemuleza Makamu wa Pili wa Rais kuwa China itaendelea kutoa mashirikiano yake kwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutokana na udugu wa kihistoria uliojengeka kwa muda mrefu sasa.

Bw. Zhang Zhisheng amesema China ni Taifa linalojali uhusiano na mataifa mbali mbali Afrika bila ya kujali utofauti wa ukubwa au udogo na mipaka ya kimaeneo, na kueleza kuwa China inaheshimu mambo ya ndani ya nchi ikiwemo masuala ya kisiasa.

Katika mazungumzo yao Balozi huyo mdogo wa China amesema mwishoni mwa mwaka huu China inatarajia kufanya mkutano mkubwa wa kimataifa utakaozishirikisha nchi mbali mbali kutoka Afrika ikiwa na lengo la kuendeleza uhusiano na ushirikiano miongoni mwa nchi marafiki.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.