Habari za Punde

BALOZI NJOOLAY AAGWA, APONGEZWA, AIMWAGIA SIFA MKURABITA KWA UCHAPAKAZI


Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Baiashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), anayemaliza muda wake, Balozi mstaafu Njoolay akicheza muziki na Mtumishi wa mpango huo, Agnes Moshi wakati wa hafla ya kuagwa kwa Bodi ya wakurugenzi iliyomaliza muda wake wa miaka mitatu, jijini Dodoma Juni 18, 2021.
Balozi mstaafu Njoolay akifurahia jambo na Mratibu wa mpango huo, CPA, Dkt. Seraphia Mgembe.
Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Baiashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), CPA, Dkt. Mgembe akizungumza wakati wa hafla hiyo, kwa kuipongeza Kamati ya Uongozi  kwa kazi nzuri na yenye mafanikio waliyoifanya wakati wa kipindi chao cha miaka mitatu ndani ya MKURABITA.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa MKURABITA, Mujungu Masyenene akiishukuru Kamati ya Uongozi inayomaliza muda wake kwa ushirikiano mkubwa walioufanya wakati wa uongozi wao.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa MKURABITA, Glory  Mbilimonya akiongoza hafla hiyo.

Sasa ni wakati wa kuserebuka.




 Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA, anayemaliza muda wake, Balozi Njoolay (aliyekaa katikati) akiwa na baadhi wajumbe wa  pamoja na baadhi ya watumishi wa MKURABITA. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

 

Na Richard Mwaikenda, Dodoma

 MWENYEKITI wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), anayemaliza muda wake, Balozi  Daniel  Ole Njoolay ameishukuru Menejimenti na watumishi wa mpango huo kwa kuwa wasikivu kutekeleza maagizo waliyokuwa wanawapatia ndani ya miaka mitatu ya uongozi wao.

Balozi Njoolay, ameyasema hayo wakati wa hafla fupi ya MKURABITA kuiaga kamati hiyo iliyoandaliwa na uongozi wa Mpango huo katika Hoteli ya Collina, jijini Dodoma.

Njoolay amesema kuwa usikivu na uchapakazi wao ndiyo umewezesha MKURABITA kuwa na mafanikio makubwa na kuwataka waendelee na moyo huo na kuisapoti kamati  nyingine itakayokuja baada ya wao kuondoka.

"Kwa niaba ya wajumbe wenzangu napenda nichukue nafasi hii kuishukuru menejimenti, mmekuwa wasikivu kwa yale maelekezo tuliyokuwa tunawapatia asanteni sana. Pili niwashukuru wajumbe wenzangu wa kamati, sijapata shida kama kiongozi walinipa ushirikiano mzuri, tunaongea vizuri, hakuna kufokeana tunaelewana na kufikia makubaliano." amesema Njoolay.

Aidha, ili kuboresha utendaji na mahusiano kazini, Balozi Njoolay ameutaka uongozi wa MKURABITA kuanzisha Family Day itakayowajumuisha viongozi, watumishi na familia zao ambapo watacheza kwa pamoja na kufahamiana zaidi.

Amesema kuwa wakifanya hivyo utendaji kazini utaongezeka bila wao kujua, lakini pia mchanganyiko huo utaongeza uhusiano miongoni mwao na kuwa wamoja.

Ametoa mfano kuwa akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo, alianzisha Family Day baada ya kuwakuta wafanyakazi hali yao ikiwa si nzuri, kitendo ambacho kiliamsha ari ya ufanyakazi na kujenga uhusiano mzuri miongoni mwao na familia zao kwa ujumla.

Pia, akiwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, baada ya kukuta hali ya utengano kati ya watumishi wa kawaida na maofisa wa ubalozi, aliamua kuanzisha Family Day, jambo ambalo lilisaidia sana kujenga umoja na utendaji kazi ukaongezeka. Alipowatangazia kuwa anarejea nchini watumishi ambao asilimia kubwa walikuwa ni wanigeria walilia machozi na kusababisha hata yeye kulia.

"Mchango wenu kwa muda wa miaka mitatu mliokuwa nasi ni mkubwa sana, si kwa kusifia tu, bali huo ndiyo ukweli, kuna vitu mmefanya vinavyotufanya sisi tufuate, Uongozi  wa kutufanya  tuwasikilize, tusikie hamu ya kutekeleza  uliyoyasema na bodi yako, tunawashukuru sana," alianza kwa kusema hayo Mratibu wa MKURABITA,CPA, Dkt Seraphia Mgembe.


CPA,Dkt. Mgembe amesema kuwa moja ya mambo aliyomuachia Njoolay atakayokumbuka daima na kuendelea nayo katika uongozi wake ni kwamba ukiwa kiongozi kabla ya kumfanyia jambo mtu mwingine au mfanyakazi wako "Lionje kwanza  ukikuta chungu usimfanyie mfanyakazi, na ukionja ukikuta tamu basi mfanyie. kwa kipindi chote  cha ufanyakazi wako Njoolay  umekuwa ukifanya hivyo," alisema Dkt. Mgembe.

"Kwa kipindi cha uongozi wenu utekelezaji wa maelekezo yenu umeleta chanya MKURABITA, tunawashukuru sana kwa uongozi wenu mwema, tunaamini huko mwendako mtakuwa mabalozi  muisemee vizuri MKURABITA ili urasimishaji usonge mbele," hayo ni maneno ya
Kaimu Mkurugenzi wa Urasimishaji Ardhi na Biashara wa MKURABITA, Jane Lyimo.

 
Naye Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa MKURABITA,
Mujungu Masyenene alisema kuwa uwepo wa kamati hiyo yenye watalaamu wengi, wamejifunza mengi na kuwafanya iwe rahisi kutekeleza malengo yao, na kwamba wataendelea kufanya mawasiliano nao ili waendelee kuchota utalaamu huo kwa lengo la kuendelea kuboresha ajenda ya urasimishaji nchini.

Kamati hiyo ambayo ilianza kazi 2018/2018 imeongoza kwa muda wa miaka mitatu hadi 2021. Kabla hapo alianza John Chiligati na kufuatiwa na aliyekuwa Spika wa Bunge, Anne Makinda.

Kamati ya Uongozi inayomaliza muda wake ni;

1. Balozi Daniel Ole Njoolay (Mwenyekiti)
2. Bi. Immaculata M. Senje
3. Bi. Ened Munthali
4. Bi. Nana R. Mwanjisi
5. Bi Ritta Magere
6. Bi. Angelista Kihaga
7. Bw. Emmanuel Mayeji
8. Bw. Agustino K. Ollal
9. Bw.Yakub Janabi
10. Bw.Salhina Mwita Ameir
11. CPA. Dkt. Seraphia Mgembe (Katibu)
12. Bi.Anna Mwasha (alistaafu 2020 utumishi akiwa mjumbe kutoka Wizara ya Fedha na Mipango)
Kamati ya Uongozi wa MKURABITA ilikuwa na jumla ya wajumbe 12' pamoja na Katibu ambaye ni Mratibu wa Mpango.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.