Na Lucas Raphael,Tabora
Mkuu wa wilaya Tabora Dkt Yahya Nawanda amewataka wazazi na walezi mkoani hapa kuwekeza kwenye elimu ya watoto wao kwani elimu ndio Nuru na mwanaga wa maisha yao ya baadaye.
Alitoa wito huo katika mahafali ya saba ya chuo cha Tabora Polytechinic College yaliyofanyka kwenye kiwanja cha chuo hicho kilichopo kata ya Mpera manispaa ya Tabora jana.
Alisema kwamba wazazi na walezi wanajukumu kubwa la kuhakikisha watoto wao wanapata elimu nzuri na bora kwani maisha bila elimu ni sawa na kukosa mwanga kwenye maisha ya utandawazi.
Aidha aliwapongeza wazazi na walezi wanaosomesha watoto wao kwa kunyima kwa kulipa ada kila baada ya muhula wa masomo kwani kufanya hivyo unamwekea mazingira na mwanga bora na nuru njema mtoto ili kuweza kufanikiwa kwenye maisha ya baadaye .
Hata hivyo mkuu huyo wa wilaya aliwataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawalinda watoto wao na kuwawekekea mazingira bora ya maisha kwa kuepukana na vishawishi vinavyoweza kusababisha kujiingiza kwenye vitendo vya kihalifu .
Alisema kwamba katu hatoweza kuona vitendo hivyo vikifanyika wilani humo badala yake wahalifu wote watakutana na mkono wa sheria .
Awali Mkurugenzi wa Chuo Cha Tabora Polytechnic College Shabani Mrutu alimweleza mkuu wa wilya hiyo ambaye alikuwa mgeni Rasmi wa mahafali hayo ya saba Dkt Yahya
Nawanda kuwa chuo hicho kina changamoto za usalama mdogo katika maeneo ya chuo nyakati za usiku.
Aidha alisema kwamba changamoto zingine ni wazazi kuwa na uwezo mdogo wa kulipa ada na kusababisha mwanafunzi kuendelea ma masomo , Lakini chuo hicho kina mipango mikakati ya chuo ni kuendelea kuwekeza kwenye wakufunzi wenye sifa, vifaa vya kufundishia na kujifunzia ili chuo kiendelee kuwa bora na kimbilio la vijana wa Tabora.
Mrutu alisema kwamba malengo mengine ni kujenga hospitali ya kisasa , kuendelea kushirikiana na jamii inayowazunguka na kutoa huduma ya afya bure kwa jamii.
Alisema chuo kimefanikiwa katika nyanja mbalimbali kutoka kwenye majengo ya kupanga na kujenga majengo ya yenyewe , kusajili chuo, kutoa wahitimu zaidi ya 1,000 na kujiunga na vyuo vikuu ndani na nje ya nchi
Alisema chuo hicho kina kozi 10 ambacho kilianzishwa ili kuitikia wito wa serikali kuzitaka sekta binafsi nchini kuwekeza elimu ya ufundi ili kuweza kuandaa wataalam watakaosaidia ukuaji wa uchumi wa sekta ya viwanda.
Mkurugenzi Mrutu alisema kwamba chuo hicho kilianzishwa mwaka 2004 kikiwa na jina la Musoma Utalii College, hapo awali kilikuwa na fani 2 ambazo ni Uongozaji wa watalii na Usimamizi wa Hoteli chini ya usajili wa VETA.
Aidha alimueleza mkuu wa wilaya kwamba hapo awali chuo hicho kilianza ma wanafunzi 42 na wakufunzi 4 na kiliendelea kukua hadi 2012 kiliposajiliwa na Baraza la Elimu ya ufundi la Taifa NACTE.
Katika mahafali hayo waliohitimu ni wanachuao 290 kutoka katika fani za Ufamasia ,Utabibu , Maabara ,Tehama Waongza watalii ,Watunza Kumbukumbu ,Waandishi wa habari na Utangazaji na Walimu wa Elimu ya Awali.
No comments:
Post a Comment