Habari za Punde

Mhe.Hemed Awaasa Wananchi Kuchukua Tahadhari na Maradhi ya Corona Yanayoendelea Kuwa Tishio Duniani.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na waumini katika Masjid Suud Regeza Mwendo huku akiwakumbusha kuachana na maneno ya Kasumba kutoka kwa watu wasiokuwa na utalamu wa masuala ya Afya.
Wamumini waliotekeleza ibada ya Sala ya Ijumaa katika Masjid Suud Regeza Mwendo wakimskiliza kwa makini Mhe. Hemed wakati akiwasalimia maara baada ya kukamilika kwa kwa sala ya Ijumaa.

Na.Kassim Abdi. OMPR.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewataka wananchi wa Zanzibar kuendelea kuchukua tahdhari juu maradhi ya Covid-19 yanayoendelea kuwa tishio Duniani.

Mhe. Hemed ameleza hayo mara baada ya kukamilika kwa ibada ya sala ya Ijumaa aliyojumuika na waumini na wananchi wa Mwera katika Masjid Suud uliopo Regeza Mwendo wilaya ya Magharibi “A” Unguja.

Amewakumbusha waumini na wananchi kwa ujumla kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maradhi hayo kwa kufuata kikamilifu maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa Afya nchini ili kujikinga na athari zitokanazo na ugonjwa huo.

Aidha, Makamu wa Pili wa Rais amewataka wananchi kuachana na maneno ya kasumba yanayotolewa na baadhi ya watu mitaani ambao hawana utalamu na masuala yanayohusina na mambo ya Afya.

“Wapo watu wanatia kasumba katika kuchukua tahadhari dhidi ya chanjo, naomba musiwasikilize” Alieleza Makamu wa Pili wa Rais

Ameleza kuwa, suala la kuchukua chanjo juu ya maradhi ya Covid-19 bado kwa upande wa serikali suala hili limendelea kuwa jambo la hiyari na hakuna mtu atakaelazimishwa lakini kwa watu wanaohitaji chanjo hiyo amewaomba kufuata taratibu zinavyoelekeza ili waweze kupatiwa huduma hiyo.

Akigusia juu ya suala la madawa ya kulevya Makamu wa Pili wa Rais amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano katika kupiga vita uwingizaji, usambazaji na utumiaji wa madawa hayo kutokana na athari mbaya zinazosababisha kupotea kwa nguvu kazi ya Taifa.

Ameleza kwamba, serikali imejipanga kutokomeza kabisa jaanga hilo kwa kuchukua hatua kali kama ilivyochukua hatua dhidi ya vitendo vya udhalilishaji ikiwemo kufanya marekebisho kwa baadhi ya sheria mbali mbali.

“Jambo hili halina msingi mzuri hapa kwetu Zanzibar” Alisema Mhe. Hemed

Pamoja na mambo mengine Mhe. Hemed amewakumbusha wananchi kuendeleza ushirikiano na mshikamano mingoni mwao ili kuunga mkono jitihada za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barza la Mapinduzi DK. Hussein Mwinyi kwani kufanya hivyo kutasaidia kuchochea kupatikana kwa maendeleo.

Nae, Khatib wa Sala ya Ijumaa Sheikh Ahmed Khamis Bilali amewakumbusha waumini kuendelea kuhurumiana katika masuala mbali mbali kwa kusaidiana na kutekeleza mambo mema kwa lengo la kupata radhi kutoaka kwa Allah (S.W).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.