Habari za Punde

Mkurugenzi TAMWA-ZNZ ataka uimarishwaji ulinzi watoto kipindi cha Skukuu.

 
Mkurugenzi wa TAMWA-Zanzibar Dkt. Mzuri Issa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandisi wa habari Ofisini kwake Tunguu.

Na Muhammed Khamis,TAMWA ZNZ.

Wakati Zanzibar na Tanzania kwa ujumla zinaungana na Mataifa mengine ulimweguni  kusherekea sikukuu ya Eid-Hajj Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanaongeza ulinzi kwa watoto wao katika kipindi chote cha Sikukuu.


Alisema Zanzibar kama sehemu nyengine za dunia watoto husherekea sikukuu kwa kwenda maeneo mbali mbali ikiwemo kuwasalimia ndugu na kwamba wapo watu wenye nia ovu hutumia mwanya huo kutimizia dhamira zao mbaya zikiwemo za kuwadhalilisha watoto kijinsia.


Alisema kikawaida  kusherekea sikukuu ni jambo zuri ambalo huleta furaha kwa watoto na wazazi wao lakini furaha hio inapaswa kuwekewa umakini zaiid ili isiharibu furaha na kuwa sehemu ya majonzi yasioweza kusahaulika daima.


Alieleza kuwa kikawaida watu wenye nia ovu huishi karibu na jamii hivyo ni rahisi kuwaona watoto wanaotembea mitaania na wanaweza kuwahadaa  ikiwa ni pamoja na kuwarubuni kwa kuwapa mkono wa eid hatimae kutenda unyama wao.


Aidha alitoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha hawawaachi watoto wao kwenda kwenye viwanja vya skukuu pekeao badala yake wawafuatanishe na watu wenye kuaminika kwani mara kadhaa wanashuhudiwa baadhi ya watoto pia kupotea na kwenda kusikojulikana.


Katika hatua nyengine aliwataka wazazi na walezi kuhakikisha wanaacha tabia ya kuwavalisha watoto nguo zisizokwenda na maadili badala yake wawavalishe nguo zinakwenda na maadili ya kizanzibar kwa lengo la kuwastiri watoto hao.


Sambamba na hayo aliliomba jeshi la polisi katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba kuongeza kasi ya ulinzi kuanzia mabarabarani ili kuepusha ajali za watoto zinazoweza kuepukika sambamba na maeneo yote ya viwanja vya sikukuu.


Wakati hayo yakijiri inaelezwa kuwa visiwani hapa matukio ya udhalilishaji yameongezeka kwa mwezi juni ukilinganisha na mwezi mei ambapo jumla ya matukio ya udhalilishaji yapatayo 97 yamaeripotiwa kwa mwezi June  wakati mwezi mei yaliripotiwa matukio 66 pekee.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa afisa kutoka ofisi ya mtakwimu mkuu wa Serikali Rahma Hassan alisema katika matukio hayo 97 kwa mwezi juni 49 ni ya kesi za kubaka, 11 kulawiti,21 kuingiliwa kinyume na maumbile, 10 kutorosha na 7 mashambulio ya aibu.


Akifafanua kuhusu mwezi mei mwaka huu alisema matukio yote yalikua  66 ambapo kwa kesi za kubaka zilikua,  43 kulawiti 7,kutorosha 7 na shambulio la aibu 9.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.