Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi akutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Taasisi Al Falasi Foundation ya UAE

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na mgeni wake Mwenyekiti wa “Foundation of Humanitarian Initiative” ya  UAE Bw.Ahmad Al Nazr Al Falasi alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza mgeni wake Mwenyekiti wa “Foundation of Humanitarian Initiative” ya  UAE Bw.Ahmad Al Nazr Al Falasi alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amekutana na kufanya mazungumzo na  Mwenyekiti wa Taasisi inayoshughulikia misaada ya Kibinaadamu kutoka Umoja wa Nchi za Kiarabu (UAE) Sheikh Ahmad Al Nazir Al Falasi na ujumbe wake.

Katika mazungumzo yake ya Taasisi hiyo, Rais Dk. Mwinyi ameihakikishia Taasisi hiyo kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kushirikiana na Taasisi hiyo katika kuimarisha huduma za kijamii pamoja na zile za kimaendeleo.

Rais Dk. Mwinyi ameipongeza Taasisi hiyo kwa utayari wake wa kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha sekta ya afya ikiwa ni pamoja na kusaidia vifaa tiba katika Hospitali  kuu za Unguja na Pemba ikiwemo Hospitali ya Mnazi Mmoja na Vitongoji Pemba.

Mapema  Sheikh Ahmad Al Nazir Al Falasi alimueleza Rais Dk. Mwinyi azma ya Taasisi anayoingoza ya kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha sekta ya afya hapa Zanzibar.

Aidha, Al Falasi alimueleza Rais Dk. Mwinyi kwamba mbali ya kuunga mkono juhudi hizo pia, amevutiwa na mazingira ya uwekezaji katika sekta ya kilimo hapa Zanzibar na kuahidi kutekeleza azma yake hiyo.   

Ujumbe huo ambao umefuatana na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui pia, unatarajia kutembelea kisiwani Pemba katika hospiitali ya Vitongoji, Chake Chake na Wete.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822  

 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.