Habari za Punde

Makatibu Wakuu wa Kamati ya Fedha, Uchumi na Biashara wa SMZ na SMT wakutana Dodoma

Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na (SMZ), Bw. Emmanuel Mpawe Tutuba (katikati) akiongoza Kikao cha Kamati ya Fedha, Uchumi na Biashara ngazi ya Makatibu Wakuu chenye wajumbe kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).  Kulia ni Dkt. Juma Malik Akil, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango na Kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Ngelela Maganga. Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 02/08/2021 katika Ukumbi wa Reform – uliopo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Wajumbe wakifuatilia mjadala wa Kikao kazi cha Kamati ya Fedha, Uchumi na Biashara ngazi ya Makatibu Wakuu kilichofanyika leo tarehe 02/08/2021 katika Ukumbi wa Reform – uliopo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.


 Wajumbe wa Kikao cha Kamati ya Fedha, Uchumi na Biashara ngazi ya Makatibu Wakuu wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukamilika kwa kikao kazi cha Maandalizi ya Kikao cha Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ ya Kushughulikia Masuala ya Muungano. Katikati ni Mwenyekiti wa Kikao hicho Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango (SMT), Bw. Emmanuel Mpawe Tutuba. Wengine katika picha, wa pili kutoka kulia ni Dkt. Juma Malik Akil, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango (SMZ) na Bw. Amour Hamil Bakari, Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi (SMZ), Bi. Mary Ngelela Maganga, Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (SMT) na Bw. Khalid Hamrani Mkurugenzi, Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali – Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.