Habari za Punde

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan Atembelea Maeneo ya Uwekezaji Nchini Rwanda Akiwa Katika Ziara Yake.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana  na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame mara baada ya kuwasili katika eneo la Uwekezaji wa kiwanda cha Inyange Plant Entrance kilichopo mjini Kigali Rwanda leo Agosti 03,2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na mwenyeji wake Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakiangalia baadhi ya Bidhaa mbalimbali zinazozalishwa katika kiwanda cha Inyange Plant Entrance mjini Kigali wakati walipotembelea kiwanda hicho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na mwenyeji wake Rais Paul Kagame wa Rwanda wakitembelea katika kiwanda cha Inyange Plant Entrance mjini Kigali kinachozalisha Juisi, Maziwa na Maji ya kunywa 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia moja ya aina ya simu zinazotengenezwa katika kiwanda cha Mara Phone Mjini Kigali Rwanda, wakati alipokua katika ziara yake ya siku ya pili nchini Rwanda leo tarehe 03 Agosti,2021. Kulia ni Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame. 

-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakipata maelezo kutoka kwa Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha CFAO MOTORS kinachotengeneza Magari aina ya Vokswagen kuhusu huduma zinazotolewa wakati walipotembelea  kiwanda hicho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame, wakiwa katika picha mbele ya Gari aina ya Volkswagen mara baada ya kutembelea kwenye Kiwanda cha kutengenezea Magari CFAO MOTORS Mjini Kigali Nchini Rwanda
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Rais Paul Kagame wa Rwanda kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Rwanda baada ya kukamilisha ziara yake ya siku mbili Nchini Rwanda
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Rais Paul Kagame wa Rwanda kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Rwanda baada ya kukamilisha ziara yake ya siku mbili Nchini Rwanda.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.