Kamnda wa Uhifadhi wa Kanda ya Magharibi kutoka Mamlaka ya ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA) Bigilamungu Kagoma akionyesha bunduki aina ya SMG ilikamatwa hivi karibuni katika doria ya kusaka majangili kwenye mapori ya akiba mbalimbali
Na Lucas Raphael,Tabora
MAMLAKA ya Usimammizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Kanda ya Magharibi imewakamata Majangili 11 wakiwa na Bunduki 11 pamoja na Gobore 31 zilizosalimishwa katika Msako Unaoendelea katika Mikoa ya Tabora na Katavi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake jana Kamanda wa Uhifadhi wa Kanda ya Magharibi Bigilwamungu Kagoma alisema Majangili hao wenye Bunduki walikamatwa Wilaya za Kaliua, Sikonge Urambo na Mlele.
Kamanda Kagoma alisema kuwa msako huo ambao ni endelevu ulianza Mapema Mwezi Septemba lengo lake ni kusaka watu wanaojihusisha na Ujangili.
Alisema miongoni mwa bunduki zilizokamatwa moja ni aina ya Short gun na Rifle iliyotengenezwa kienyeji ambazo zilikutwa majumbani mwa majangili wawili.
Aliongeza kuwa kati ya majangili hao mmoja alikutwa kijiji cha Mibono Wilaya ya Sikonge akiwa na bunduki aina ya Rifle 30 06.
Kamanda Kagoma alisema kuwa jangili wa pili alikutwa na Shortgun akiwa ndani ya Hifadhi ya Jumuiya ya Uyumbu Wilaya ya Urambo pia alikamatwa na maganda 15 ya risasi za buinduki na Baruti Gm 200.
Alisema kuwa jangili mwingine alikutwa na Gobore aliweza kuwaonyesha Kiwanda chake cha Kutengenezea Bunduki hizo na vifaa mbali mbali ndani ya Pori jipya la akiba la Inyonga.
Kufuatia hali hiyo aliwaonya wanaojihusisha na Ujangili kuacha vitendo hivyo mara moja pamoja na wanaomiliki bunduki kinyume cha sheria kuzisalimisha kabla hawajakamatwa na kuchukuliwa hatua kali.
Kamanda kagoma pia alitoa wito kwa wananchi waliokuwa wanatumia Mapori ya Inyonga, Wembele na Igombe watoke mara moja kwa kuwa yamepandishwa hadhi na kuwa mapori ya Akiba kwa sasa yanamilikiwa na Tawa.
No comments:
Post a Comment