Habari za Punde

EJAT Yaongeza Kundi la Habari za Ushirika.

Afisa Programu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Paul Mallimbo akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Tanga kuhusu  kuongezwa kwa kundi la Habari  za Ushirika  katika Tuzo za Umahiri za Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2021,   kulia ni Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tanga Henjewele John.

Na.Oscar Assenga - TANGA.
BARAZA la Habari Tanzania (MCT) kwa niaba ya Kamati ya Maandalizi ya Tuzo za Umahiri za Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2021, limetangaza kuongezwa kwa kundi moja la kushindaniwa na kufanya makundi yanayoshindaniwa kwa sasa kuwa 19.

Akitangaza kuongezwa kwa kundi hilo kwa waandishi wa Habari mjini Tanga,Afisa Programu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Paul Mallimbo alisema kuongezwa kwa kundi hilo kunafuatiwa na ombi la Tume ya Maendeeo ya Ushirika Tanzania (TCDU) ya kutaka kuwa na kundi ambalo litahusisha habari za vyama vya ushirika nchini,ikiwa ni pamoja na vyama vya ushirika.

Alisema kundi lililoongozwa ni tuzo ya uandishi wa Habari za Ushirika, ambalo wakati wa mashindano litatazamwa katika vigezo vile vile vinavyotumika kwenye makundi mengine.

“Kama mtakumbuka tuzo hizo zilizinduliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu,Mhe Joseph Sinde Warioba, wakati wa kilele cha tuzo za 2020,Septemba 10,2021 zilizofanyika Jijini Dar es Salaam”Alisema Mallimbo.

Alisema katika makundi mengine yatakayoshindaniwa katika tuzo hizo ni Tuzo ya uandishi wa habari za uchumi, Biashara na fedha, Tuzo za Uandishi wa habari za Michezo na Utamaduni, Tuzo ya Uandishi wa Habari za Kilimo na Biashara ya Kilimo, Tuzo ya Uandishi wa Habari za Elimu, Tuzo ya Uandishi wa Habari za Utalii na Uhifadhi, Tuzo ya Uandishi wa Habari za Uchunguzi na Tuzo ya Uandishi wa Habari za Data.

Aidha aliyataja makundi mengine yanayoshindaniwa ni Tuzo ya Uandishi wa Habari za Haki za Binadamu na Utawala Bora,Mpiga Picha Bora wa Magazeti,Mpiga Picha Bora wa Runinga,Mchora Katuni Bora,Tuzo ya Uandishi wa Habari za Jinsia na watoto,Tuzo ya Uandishi wa Habari za Gesi,Mafuta na Uchimbaji wa Madini.

Aidha alizitaja tuzo nyengine kuwa ni Tuzo ya Uandishi wa Habari za Walemavu,Tuzo za Uandishi wa Habari za Afya,Tuzo za Uandishi wa Habari za Sayansi na Teknologia,Tuzo za Uandishi wa Habari za Hedhi Salama,Tuzo ya Uandishi wa Habari za Ushirika na Kundi la Wazi.

Hata hivyo alisema kamati ya maandalizi ya EJAT inayoongozwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) na washirika wake ni pamoja na mfuko wa vyombo vya habari Tanzania (TMF),Taasisi ya vyombo vya Habari kusini mwa Afrika –Tawi la Tanzania (MISA-TAN),Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA),Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF),Haki Elimu,SIKIKA na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.