Habari za Punde

Jukwaa la kwanza la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Italia lfanyika kwa mafanikio

 



Jukwaa la kwanza la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Italia limefanyika Jijini Roma kwa mafanikio makubwa, Italia na kuwakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji zaidi ya 250 kutoka nchi zote mbili hasa katika kipindi hiki cha Uviko 19.

Pamoja na mambo mengine, jukwaa hilo limewawezesha wafanyabiashara na wawekezaji kujadili fursa, uwezekano wa ubia, changamoto zinazokabili mazingira ya biashara na njia ya kuboresha mahusiano ya kibiashara kati ya Tanzania na Italia ambapo limendaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Italia kwa kushirikiana na Kituo cha Taifa cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Mamlaka ya Taifa ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA).

Ujumbe wa Tanzania umeongozwa na Naibu Waziri wa Madini, Prof. Shukrani Manya ambapo Prof. Manya amewaeleza wawekezaji na wfanyabiashara kutoka Italia kuwa Tanzania kwa sasa imejikita kuwekeza katika miundombinu wezeshi ya uwekezaji, na kwamba hilo ndilo jambo ambalo Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Rais Samia ameliweka suala la uwekezaji kama kipaumbele katika kuhakikisha kuwa wawekezaji kutoka nje na ndani ya nchi wanawekeza fedha na mitaji yao ili kukuza biashara na ajira kwa watanzania na kuwezesha uchumi wa Tanzania kusonga mbele

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.