Habari za Punde

Kongamano la siku 16 za kupinga udhalilishaji likiendelea kisiwani Pemba

BAADHI ya wanafunzi kutoka vyuo mbali mbali vikuu Kisiwani Pemba, wakipitia katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 wakati wa uwasilishaji wa mada juu ya Haki za Binaadamu, Dhana ya Udhalilishaji, kwenye kongamano la siku 16 za kupinga udhalilishaji kwa wanafunzi hao, lililoandaliwa na kituo cha Huduma za Sheria Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

AFISA Mipango kutoka kituo cha huduma za sheria Zanzibar Tawi la Pemba, Safia Saleh Sultani akiwaonyesha wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo Pemba, katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 wakati wa kongamano la siku 16 za kupinga Udhalilishaji kwa wanafunzi hao.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

AFISA Mdhamini Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ zanzibari, Thabit Othman Abdalla akifungua kongamano la siku 16 za kupinga udhalilishaji, lililoandaliwa na kituo cha huduma za sheria Zanzibar Tawi la Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

MWANASHERIA kutoka Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Tawi la Pemba, Siti Habibu Mohamed akizungumza na Mwaandishi wa habari Fatma Hamad Faki (Pemba yaleo) na Zuhura Juma (Zanzibarleo), baada ya kumaliza utoaji wa elimu kwa wanafunzi wa skuli ya Madungu Msingi juu ya siku 16 za kupinga udhalilishaji wa kijinsia.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.