Habari za Punde

Timu ya Baraza la Wawakilishi yatakiwa kujenga heshima na kurudisha hadhi ya michezo Zanzibar

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zubeir Ali Maulid akitoa maelekezo  na ushauri kwa wachezaji wa timu ya Baraza la Wawakilishi kuelekea katika mchezo wao wa mashindano ya Mabunge ya Afrika mashariki  unaotarajiwa kuchezwa siku ya Jumanne

 Wachezaji wa Timu ya Baraza la Wawakilishi wakiwa katika mazoezi uwanja wa DON BOSCO Jijini Arusha kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya Mabunge ya Afrika Mashariki yanayotarajiwa Kufunguliwa tarehe 6 Disemba.


Spika wa Baraza la Wawakilishi  Mhe Zubeir Ali Maulid amewasisitiza wachezaji wa timu ya Baraza la Wawakilishi kuitumia vyema fursa waliyoipata ya kushiriki katika mashindano ya mabunge ya Afrika Mashariki katika kujenga heshima na kurudisha hadhi ya michezo ya  Zanzibar.

 

Mhe Zubeir ameyasema hayo wakati akizungumza na wachezaji wa timu hiyo huko katika kiwanja cha DON BOSKO jijini Arusha wakati timu hiyo ikiendelea na mazoezi ya kujiweka sawa katika mashindano hayo yanayotarajia kufunguliwa rasmi tarehe 6 disemba.

 

Amesma timu za Baraza la wawakilishi ni miongoni mwa timu zinazoonyesha kandanda zuri ambalo huwafurahisha mashabiki wa Zanzibar na wageni hatua inayowapa moyo wachezaji kuendelea kujituma Zaidi kuhakikisha wanaitangaza vyema Zanzibar katika michezo yote waliyoshiriki.

 

Aidha amemshukuru spika  Wa Bunge la Afrka Mashariki pamoja na viongozi wengine wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana vyema na baadhi ya viongozi wa timu ya Baraza la wawakilishi kuhakikisha kuwa Zanzibar nao wanakua ni sehemu ya mashindano hayo.

 

Mapema mwenyekiti wa timu ya Baraza la Wawakilishi mhe Hamza Hassan Juma amemuhakikishia Spika zubeir kwamba timu hiyo ipo imara na ipo tayari kwa mashindano kutokana na maandalizi mazuri waliyojiandaa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.