Habari za Punde

kilele cha mkutano wa RewirEd unaojadili namna ya kuboresha elimu

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akisikiliza mada mbalimbali zilizowasilishwa kwenye Ukumbi wa Kaskazini (North Hall) kwenye viwanja vya Maonesho ya Dubai (Expo2020), mjini Dubai, Falme ya Nchi za Kiarabu, kuhusu namna dunia inavyoweza kuboresha elimu na ujuzi kwa vijana pamoja na kujadili mikakati ya kupata rasilimali fedha, ujulikanao kama RewirEd. Kulia kwake ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na kushoto kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali.

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akiwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali, wakati wa kilele cha mkutano wa RewirEd unaojadili namna ya kuboresha elimu, unaofanyika Mjini Dubai, Falme za nchi za Kiarabu.
RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizunguza jambo na Mshauri wa Masuala ya elimu kutoka Taasisi ya uchapaji ya ALPHA, Bi. Zainab Jarir, wakati wa kilele cha mkutano wa RewirEd unaojadili namna ya kuboresha elimu, unaofanyika Mjini Dubai, Falme za nchi za Kiarabu, mbao Mhe. Kikwete, Waziri wa Elimu na Sayansi Prof. Joyce Ndalichako (Mb) na Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wamealikwa ambapo Prof. Ndalichako anatarajiwa kuzungumza kuhusu masuala ya elimu nchini Tanzania tarehe 14 Disemba, 2021.

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akifurahia jambo na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali, wakati wa kilele cha mkutano wa RewirEd unaojadili namna ya kuboresha elimu, unaofanyika Mjini Dubai, Falme za nchi za Kiarabu.

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Tanzania kutoka Wizara ya Fedha na Mipango ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa pili kulia) wakati wa kilele cha mkutano wa RewirEd unaojadili namna ya kuboresha elimu, unaofanyika Mjini Dubai, Falme za nchi za Kiarabu. Kushoto ni Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje-Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Robert Mtengule.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango-Dubai)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.