Habari za Punde

Balozi Mahmoud Thabit Kombo akutana na NGO za Kitaliano


 Na. Mwandishi Wetu, Italy.


BALOZI wa Tanzania,  nchini Italy, Mhe Mahmoud Thabit Kombo amepongeza juhudi za Taasisi binafsi zisizo za Kiserikali (NGO's) za kimaendeleo zinazosaidia jamii kwani zinatoa michango mikubwa ya Kibinadamu kwa Tanzania, ikiwemo kukuza mahusiano ya muda mrefu yaliopo kati ya nchi hizo mbili.


Balozi Kombo amebainisha hayo katika hafla iliyofanyika jioni ya Februari 26,2022, ambapo inakuwa ni mara ya kwanza kukutana na NGO's hizo zaidi ya 65 za Kiitaliano zinazofanya kazi zake nchini Tanzania pamoja na kupokea Ripoti mbalimbali za Miradi iliyofanikiwa kwa kiasi kikubwa.


Mhe Balozi Kombo amewahakikishia na kuwahidi kufanya kazi kwa karibu na Mamlaka husika ili kutatua changamoto zilizokuwepo katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo inayofanyika na inayotarajiwa kufanyika nchini Tanzania.

Awali, Mhe. Balozi Kombo alipokea Kitabu rasmi kilichoandikwa na NGO ya Zawadi kutoka nchini Tanzania, ambayo ina Kituo chake cha kulea Mayatima na Watoto wenye Ulemavu.


Ambapo pia, NGO hiyo ya Zawadi ilipata wasaha wa kuonesha Filamu na Kitabu cha hatua na mafanikio yaliyofanikiwa katika Mkoa wa Iringa nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.