Habari za Punde

Mawakala wa Ezypesa wanolewa Wakumbushwa kuzingatia sheria za utoaji huduma

1.     Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Zantel, Moses Alphonce akizungumza wakati wa semina ya uboreshwaji wa huduma ya Ezypesa iliyoandaliwa na kampuni hiyo (Zantel) inayojulikana kama Ezypesa Forums 2022.Kushoto kwake ni Anne Killindu na Suleiman Salum Abdalla (kulia) ambao ni Maafisa wa Ezypesa.

1.   Baadhi ya mawakala wa Ezypesa wakifuatilia semina ya uboreshwaji wa huduma za Ezypesa iliyoandaliwa na kampuni hiyo (Zantel) inayojulikana kama Ezypesa Forums 2022.

1.     Afisa wa huduma ya Ezypesa, Eunice Hubert akitoa taaluma kwa mawakala wa Ezypesa katika semina ya uboreshwaji wa huduma za Ezypesa iliyoandaliwa na kampuni hiyo (Zantel) inayojulikana kama Ezypesa Forums 2022.Kushoto kwake ni Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Zantel, Moses Alphonce.

Zanzibar.February 2022.Kampuni ya simu za mkononi Zantel, imeendesha mafunzo kwa mawakala wake yenye lengo la kuwakumbusha kuzingatia sheria pamoja na taratibu za utoaji wa huduma ya kifedha ya Ezypesa ili kuongeza ubora wa huduma hiyo kwa wateja.

Hayo yalibainishwa katika mkutano na mawakala wa Ezypesa uliolenga kuwanoa mawakala juu ya kanuni na namna bora ya utoaji huduma kwa wateja uliofanyika Unguja-Kiembesamaki.

Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Zantel, Moses Alphonce alisema lengo kubwa la mafunzo hayo ni kuwapa mawakala ujuzi juu ya sheria za nchi, ujuzi juu ya masuala ya wizi mtandaoni pamoja faida za kuwa wakala wa Ezypesa.

Mkuu huyo alisemaa kampuni hiyo inawajibu mkubwa wa kuweka mazingira salama kwa wafanyabiashara hao ikiwamo kusimamia utekelezaji  wa sheria za nchi.

“Katika uendeshaji wa huduma hii kuna mambo mbalimbali ambayo yanatakiwa kuzingatiwa ikiwamo kwa Mawakala wetu, tunachokifanya leo ni kuhakikisha mawakala wanakuwa na ujuzi wa kutosha juu ya sheria, taratibu za utoaji huduma,” alisema.

Mbali na hayo, Kampuni hiyo inatoa  tuzo kwa mawakala wanaofanya vizuri.

Kwa upande wa Afisa wa Huduma za Ezypesa,Eunice Hurbet alisema mkutano huo unafanyika kila mwaka kwa mawakala wao ili kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili pamoja na kuleta ufanisi katika utekelezaji wa wajukumu yao.

Alisema mawakala hukutana na changamoto kadhaa katika kazi zao ambazo husababisha kutofikia malengo yao hivyo kupitia kongamano hilo husaidia kutoa mchango mkubwa wa kutatua changamoto hizo.

“Tumekuwa tukiangalia namna mbalimbali za kuboresha huduma hii ya Ezypesa ili kuwarahisishia wateja kuzitumia kwa urahisi pamoja na kuwaondoshea usumbufu,” alisema.

Mafunzo hayo yatatolewa kwa mawakala walioko Unguja, Pemba, Mtwara, Tanga, Lindi pamoja na Dar es Salaam.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.