Habari za Punde

Ziara ya Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Kijini Makunduchi.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Zanzibar, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, leo Machi 12, ameweka jiwe  la msingi pamoja na kupandisha bendera katika tawi la 'ACT Kijini Makunduchi'.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo ambae pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman akizungumza na Wanachama wa ACT Wazalendo Kijini Makunduchi akiwa katika ziara yake leo 12-3-2022.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Zanzibar, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, leo Machi 12, ameweka jiwe  la msingi pamoja na kupandisha bendera katika tawi la 'ACT Kijini Makunduchi'.

Mhe. Othman ameyafanya hayo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kuimarisha Chama katika majimbo ya Zanzibar.

Tawi jipya la Kijini Makunduchi lenye idadi ya  wanachama 122, awali ilikuwa barza ya vijana wa chama hicho iliyotambulika kwa jina la 'ISMAIL JUSA BARZA' iliyopo katika jimbo la Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja.

Ziara hio inaendele ikiwa leo ni zamu ya jimbo la Makunduchi na Paje.

Kitengo cha Habari

Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

12/03/2022.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.