Habari za Punde

Mradi wa kituo kikubwa cha Biashara na Mikutano eneo la Fumba


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk.Hussein Ali Mwinyi  amepokea Taarifa ya Muelekeo wa Ujenzi wa Miradi miwili mikubwa itakayotekelezwa Zanzibar,ambapo kwa upande wake ametoa Shukurani kwa  Mifuko mitano ya Hifadhi ya Jamii Tanzania kwa Hatua huyo iliyofikiwa.

 Miradi hio ambayo inayotarajiwa kutekelezwa ni ujenzi wa kituo kikuu cha Mabasi eneo la Kijagwani pamoja na kituo kikubwa cha Biashara na Mikutano eneo la  Fumba. 

Rais Dk.Mwinyi amesema hii ni mara ya kwanza kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii iliyokuwepo upande wa Jamhuri ya Muungano kuwekeza Zanzibar nakueleza kuwa hilo ni jambo muhimu kwa kuimarisha Muungano,kwa kuimarisha Biashara na Uchumi Mpya unaotarajiwa kujengwa.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema kuwa katika Nchi nyingi duniani Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ndio inayoendesha Uchumi wa Nchi ambapo ameongeza kuwa kwa Zanzibar anataka hali iwe kama hivyo.

Kuhusu suala la Ujenzi wa Kituo cha Mabasi cha Kijangwani, Rais Dk.Hussein Ali Mwinyi ameuhakikishia Ujumbe huo kuwa kwa Upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itahakikisha kwa Muda mfupi kadri itakavyowezekana kuweka sawa yale yote ambayo yanatakiwa kuwekwa sawa.

 Nae Mwenyekiti wa Umoja waMifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania, Masha John Mshomba, wakati akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumaliza mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti baada ya kuwasilisha Taarifa yao kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi Ikulu Zanzibar juu ya utayari wao katika kutekeleza miradi hiyo. 

Alisema tathmini ya madi wa kituo cha daladala umeshakamilikana pale serikali itakapokamilisha taratibu za kuwakabidhi eneo hilo basi kazihiyo itaaza utekelezaji mara moja.

Aidha alisema eneo hilo litakapokamilika litakuwana maduka 131, maeneo ya kuegesha gari 135, mabasi mabasi 70, ATM 10, maduka yavyakula matatu na huduma nyengine muhimu.  

Alifahamisha kuwa mradi huo utahusisha pia ujenziwa vituo vidogo vya mabasi katika eneo la Mnazimmoja na Malindi kwa ajili yakuwaleta wananchi maeneo ya mjini.

Alisema mradi huo utakapokamilika utaondosha keroya gari kuegeshwa barabarani na litakuwa ndoto kwa Zanzibar.    

Mwenyekiti huyo alisema mradi mwengine ni mradi wakituo cha biashara na Mikutano katika eneo la Fumba lakini bado unatakiwakufanyiwa tatmini zaidi.

“Mradi huu bado tunataka kuufanyia tatmini zaidi natumemuomba Rais Mwinyi atupe muda kidogo ili kufanya tathmini hii na mradi huuutakapokamilika utakuwa na faida kubwa kwa Zanzibar kwani kwa sasa hakuna kituohichi cha kimataifa cha kisasa kwa Tanzania,” alisema.    

Walimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti waBaraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kuwapa nafasi ya kushirikikatika miradi mengine ya kimaendeleo hapa nchini na waliahidi kuiangalia natathmini itakapoonesha kwamba miradi hiyo kuitekeleza basi hawatasita kufanyahivyo.

“Leo ni siku muhimu kwetu kwa kuona kwambatunakuwa ni sehemu ya mikakati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikaliya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuhakikisha tunasogeza mbele gurudumu lamaendeleo hususan kuwekeza katika miradi hii ambayo mifuko yetu mitano itaonainafaa kwa uwekezaji.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), Dk. Huda Ahmed Yussuf, alisema mradi huo kwa kiasikikubwa utaweza kupunguza changamoto ya msongamano wa magari barabarani ikiwemoeneo la skuli ya Kiswandui na Michenzani.

Alisema katika kituo hicho kutakuwa na usafirimaalum utakaotumika kwa ajili ya kuwapeleka wananchi mjini kwa kutumia mabasi yakisasa ambayo yatatumia umeme na gesi.

Dk. Huda, alisema mradi huo wa kituo cha kisasacha Mabasi Kijangwani unatarajia kutumia zaidi ya shilingi bilioni 14 hadikukamilika kwake. 

Aliwaomba wananchi wa Zanzibar kushirikiana katika kuona mradi huo unakamilika ili kubadilisha haiba ya Mji wa Zanzibar na kuwekamazingira mazuri ya usafiri wa umma. 

Imetayarishwa na Kitengo cha Habari

Ikulu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.